20 Mar 2017

Kimenukaa.. Aliyesoma Pamoja na Makonda Chuo cha Ushirika Moshi Aibuka na Haya..Amtaka Ajiuzulu Haraka Kabla Mambo Hayajazidi Kumuharibikia..!!!!


Hapa sikutaka kumzungumzia kabisa Makonda hata nilipokuwa Dodoma kwenye mkutano baadhi ya marafiki tuliosoma nae ushirika tulijadili na kuona chama kinamlea vibaya sana.

Leo nimeona video ikimuonyesha akivamia ofisi za clouds Tv hili jambo ni gumu sana sana Mhe. Rais aliangalie kwa kina sana la sivyo linaendelea kutuchafua sana, ukitazama mitandao ya kijamii utaona tunavyotukanywa na mtu anayeonekana mbaya ni Rais wangu.

Nemeona mandiko baadhi ya makada wenzangu wabunge na hata mawaziri wakishanga jambo hili, mimi binafsi nimeshindwa kuvumilia namuomba Rais wangu na mwenyekiti wangu wa ccm amuondoe Poul Makonda kwenye nafasi hii ya mkuu wa mkoa kuendelea kumwacha ni kukichafua chama chetu.

Makonda Ondoka Mwanyewe kaka yangu na rafiki yangu ondoka mwenyewe kuendelea kubaki ni kuifanya ofisi ya Rais inapoteza dira yake na mwelekeo.

ni mimi

Meijo Laizer 
Mjumbe wa NEC TAIFA
Wilaya ya Siha


Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD


Tazama Jinsi Rosa Ree na Emtee Walivyoshtua Watu...Huwezi Amini:

Share:
Weka Maoni yako Hapa

Total Pageviews


Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger