Kimenukaa...Familia ya Makonda Yaanika Ukweli Wote Juu ya Jina la Bashite,Wadai ni Lake Kabisa,Wamshangaa Kujiita Paul,Wadai Toka Apate Madaraka Kawasusa Huko Kijijini..!!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mzee Khamesse
Kutokana na kuwepo kwa taarifa za Paul Makonda kulelewa katika familia ya aliyekuwa Meya wa Jiji la Mwanza, Seleman Khamesse, JAMHURI limefika nyumbani kwa Mzee Khamesse, katika eneo la Nyamanoro, jijini Mwanza na kufanya mahojiano;

JAMHURI; Kuna taarifa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewahi kuishi nyumbani kwako. Je, ni kweli?

KHAMESSE; Ni kweli Daudi alikuja kwangu akiwa darasa la tano akitokea kijijini kwao, Koromije na kisha kuishi hapa na familia yangu.

JAMHURI; Mbona unasema uliishi na Daudi wakati nimekuuliza kuhusu Paul Makonda?

KHAMESSE; Ni kweli nimesema Daudi kwa sababu namfahamu kwa jina hilo. Amekuja kwangu akitokea kwa wazazi wake waliokuwa wakiishi Koromije, na jina lake ni Daudi Albert Bashite.

Wakati shangazi yake ambaye ni mke wangu mdogo (Mama Khamesse) anamleta hapa alikuwa akitumia jina hilo na hata alipopelekwa shule alikuwa akitumia jina la Daudi Bashite wakati anasoma Shule ya Msingi Nyanza.

Hata wakati anakwenda kuanza shule Pamba Sekondari alienda kwa jina la Daudi Bashite.

JAMHURI; Una uhusiano gani na Daudi?

KHAMESSE; Daudi ana uhusiano na mke wangu mdogo Bernadeta maarufu kama Mama Khamesse. Mama ndiye aliyemleta hapa kwani ni shangazi yake anaweza kukwambia zaidi kuhusu hilo.

JAMHURI; Tangu alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na kisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mmekuwa mkiwasiliana?

KHAMESSE; Hatuna mawasiliano kwani tangu ateuliwe amewahi kufika nyumbani kwangu hapa tulipo mara mbili tu, tena alikuja usiku.

Mara ya kwanza alikuja saa saba usiku, hakuingia ndani aliishia nje akaongea na vijana wenzie akaondoka. Mwaka jana mwezi wa Ramadhan alikuja saa tano usiku akiwa amesindikizwa na vijana wawili hakuingia ndani aliishia nje akaongea na vijana wenzie, kwa vile nilikuwa sijalala tulisalimiana akanipatia mawasiliano yake kisha akaondoka.

Ukweli ni kwamba hatuna mawasiliano, kutokana na kwamba haoneshi kuhitaji kuwasiliana kwani namba alizonipatia nikipiga hapokei, hata nilipotuma ujumbe hakukuwa na majibu.

Ila wasiliana na shangazi yake anaweza kukueleza zaidi maana mie sikukaa naye sana kutokana na majukumu yangu yaliyokuwa yakinikabiri wakati huo. Pamoja na kwamba alikuwa akiishi nyumbani kwangu.

Ramadhani Khamesse
Ramadhani ni mtoto wa Mzee Khamesse, ambaye alikuwa akisoma shule moja na Paul Makonda, amesema kwamba amesoma na kuishi na Makonda katika kipindi chote alichokuwa nyumbani kwao.

“Tulikuwa naye shule moja ya Nyanza, na jina lake ni Daud Albert Bashite. Dada yangu, mimi, huyu Daudi tulikuwa tunalala naye chumba kimoja hivyo namfahamu. Pia tulikuwa rika moja hivyo hata michezo yetu ilifanana ingawa tulikuwa tunatofautiana baadhi ya tabia,” amesema Ramadhan.

Akimuelezea Makonda amesema anajua kuishi na watu pale anapohitaji jambo lake lifanikiwe kwani alikuwa anajua kunyenyekea kwa walimu ingawa alikuwa na tabia ya kubagua marafiki hasa wale ambao familia zao zilikuwa duni. “Alikuwa ni rafiki wa wenye uwezo,” amesema.

Pia ameeleza kwamba baada ya kujiunga na masomo ya jioni Pamba Sekondari alihamia kwa ndugu yake mwingine anayefahamika kwa jina la Mwana Zakhia.

Kuhusu mawasiliano kati yao, amesema ingawa wamekua pamoja hakuna mawasiliano yoyote kati yao kutokana na Makonda kumpatia namba ambazo hata akipiga simu hazipolewi.

“Alikuja hapa mara mbili usiku tukazungumza mambo mengi ikiwa ni pamoja na kukumbushana maisha tuliyoishi. Zaidi ya hapo hatuna mawasiliano kabisa zaidi ya kumsikia na kumuona kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,” amesema Ramadhani.

Mama Khamesse
JAMHURI lilifika nyumbani kwa Mama Khamesse Lumara na kufanya mahojiano;

JAMHURI: Una uhusiano gani na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam?

MAMA KHAMESSE: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ni ndugu yangu kwani baba yake, Mzee Albert Bashite ni binamu yangu. Kwa hiyo Daudi ananiita mimi shangazi.

JAMHURI: Unaweza kunisaidia jila lake ni Daudi au Paul Makonda?

MAMA KHAMESSE: Mimi ninamfahamu kwa jina la Daudi Albert Bashite. Na hata wakati nampeleka kuanza shule katika shule ya mshingi Nyanza aliandikishwa kwa jina la Daudi Bashite.

JAMHURI: Ilikuwaje ukaanza kuishi naye?

MAMA KHAMESSE: Mama yake alikuja kuniomba mtoto wake aje kuishi na kusomea kwangu. Ukweli sikuona sababu za kumkatalia. Nilimkubaliana na kumpokea kisha ‘kumfanyia mpango wa kujiunga’ na shule ya Nyanza ambapo aliingia darasa la tano mpaka alipomaliza darasa la saba.

JAMHURI: Alipomaliza darasa la saba matokeo yake yalikuwaje?

MAMA KHAMESSE: Ukweli ni kwamba hakubahatika kufaulu ili kujiunga na kidato cha kwanza hivyo alilazimika kuanza kusoma masomo ya jioni katika shule ya sekondari ya Pamba.

Lakini hakuweza kukaa nyumbani kwangu kwa kipindi kirefu baada ya kuanza kusoma Pamba kutokana na sababu ambazo siwezi kukuelezea, kwani nilimuita mama yake tukazungumza kisha akamchukua na kumuhamishia kwa ndugu mwingine ambaye ni baba yake mdogo na Daudi.

Hata hivyo, wakati shangazi yake akigoma kutaja chanzo cha Makonda kuondoka kwa Mzee Khamesse, habari za uhakika ambazo familia ya Khamesse haikuthibitisha wala kukanusha zinasema Makonda alikuwa anachezea bunduki ya Mzee Khamesse risasi ikafyatuka na kupasua paa.

“Mzee Khamesse alisema huyu mtoto andoke haraka. Alisema kama amechezea bunduki yake kuna hatari anaweza akaua watoto wake kwa risasi kupitia michezo yake isiyokubalika,” kinasema chanzo chetu.

Mtu aliyeko karibu na Makonda amekiri lilitokea tukio hilo, ila akasema: “Hiyo ilikuwa michezo ya watoto. Mbona wengi tumemwaga uji wa mgonjwa? Ni hawa watu wa dawa za kulevya tu wanaochochea hata hayo mambo madogo.”

JAMHURI: Je, alimaliza masomo yake ya sekondari na kuhitimu?

MAMA KHAMESSE: Mh! Hapo kwenye kumaliza sekondari siwezi kukueleza lolote maana ni kautata kidogo kwani sikumbuki kitu kama hicho.

Ila ninachofahamu ni kwamba alianza kufanya kazi ya ukondakta wa daladala kwenye mabasi ya baba yake mdogo ambaye kwa sasa ni marehemu anayefahamika kwa jina la Mabina.

Baada ya muda kupita nilisikia kuwa amejiunga na Chuo cha Uvuvi Nyegezi, jijini Mwanza, na baadaye nikasikia yuko chuo huko Mbegani, Bagamoyo anasoma.

Lakini muda haukupita sana ndipo nikasikia kuwa amekuwa muhubiri hivyo alikuwa akihubiri injili na alikuwa akisafiri sana.

JAMHURI: Katika kipindi chote hicho uliwahi kusikia kuwa amebadili jina na kuitwa Paul?

MAMA KHAMESSE: Hapana nilikuwa sijawahi kusikia akiitwa jina zaidi ya tunalolifahamu wanafamilia la Daud Bashite. Na siku zote namfahamu kwa jina hilo hilo ingawa nilikuja kushangaa kuona kwenye luninga wakati yuko Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) alipotambulishwa kwa jina la Paul Makonda.

Nilishangaa jina nikadhani wamekosea, lakini kila siku zinavyokwenda niliendelea kumuona kwenye luninga akitambulishwa kwa jina la Paul Makonda huku akiwa ni Daud Bashite ninayemfahamu.

JAMHURI: Hili jina la Makonda unadhani amelitoa wapi?

MAMA KHAMESSE: Jina hili la Makonda ni jina ambalo lipo katika ukoo, upande wa babu na bibi zake, hivyo sio jina jipya katika ukoo. Lakini suala la yeye kuanza kuitwa hivyo labda yeye binafsi au wazazi wake wanaweza kulisema hilo.

Ndugu

Mmoja wa ndugu zake wa karibu (jina linahifadhiwa) amesema kwamba Daudi alishindwa kuendelea kuishi nyumbani kwa shangazi yake (Mama Khamesse) kutokana na tabia ya kupenda kuwa karibu na marafiki wenye uwezo mkubwa jambo lililokuwa linamnyima uhuru kwani alikuwa na tabia ya kuhamia huko na kutorudi nyumbani.

“Daudi alikuwa anaweza kutoka nyumbani kwao Nyamanoro akahamia nyumbani kwa rafiki zake baada ya siku kadhaa akarudi nyumbani tena kwa shangazi yake. Tabia hii ilimkera Mama Khamesse ikamlazimu kuwasiliana na wazazi wake ambao walimuondoa hapo na kumpeleka kwa ndugu mwingine,” amesema.

Amesema Mzee Albert Bashite alibahatika kuzaa watoto wawili tu ambao ni Daudi na mdogo wake wa kike ambaye hata hivyo alifariki akiwa mdogo, hivyo Daudi ni mtoto wa pekee wa Mzee Daudi Bashite na Susan Daud Malagila. Jina la Daudi alilithi kutoka kwa babu yake mzaa mama.

Shule ya Msingi Nyanza
JAMHURI lilifika Shule ya Msingi Nyanza na kukutana na Mwalimu Mkuu ambaye alikataa kujitambulisha kwa jina kwa madai kuwa hawezi kuzungumza chchote mpaka atakapopata kibali kutoka kwa wakubwa wake.

JAMHURI: Mimi ni Mwandishi wa Habari kutoka Gazeti la JAMHURI. Nimefika kwako kupata ufafanuzi kuhusiana na taarifa za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kusoma katika shule yako ya Nyanza.

Mwalimu Mkuu: Siwezi kuzungumzia suala lolote linalohusu jambo hilo. Unatakiwa kuwa na kibali kutoka Ofisi ya Mkoa, nenda kwa RAS (Katibu Tawala wa Mkoa), RAS akishatoa kibali kitatakiwa kuthibitishwa na DAS (Katibu Tawala wa Wilaya), kisha utakipeleka kwa Afisa Elimu Wilaya, ambaye naye atakithibitisha na kukuelekeza kwa Mkurugenzi wa Wilaya ambaye atakupatia kibali cha kuja nacho hapa shuleni niweze kukujibu maswali yako.

Hapa unataka data (takwimu), na taratibu za kupata data unazifahamu. Hivyo siwezi kabisa kukusaidia chochote. Karibu tena.

JAMHURI limefanya mahojiano na mmoja wa walimu shuleni hapo (jina linahifadhiwa) ambaye amethibitisha Daudi Bashite kusoma katika shule ya Nyanza.

“Nashangaa hili jambo kukuzwa kiasi hiki! Hili suala lipo wazi kabisa, Daudi au Makonda kama anavyoitwa alisoma hapa na huyo Mwalimu Mkuu wa Nyanza, Jovenary anaweza kuwa anafahamiana naye kama hakumtangulia darasa kwani naye alisoma hapa hapa. Picha unayoiona kwenye mitandao Daudi aliipigia palee kwenye ngazi,” amesema Mwalimu huyo. 

Source: Jamhuri.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ok, so what, kwani mwenyewe alishakataa ama kukubali hayo yote?

    ReplyDelete
  2. Kama nimeelewa vizuri, hata hilo jina la Makonda ni la kwao, inawezekana alipofeli akarudia kwa jina hilo..........khaaa, PEKU-PEKU KAZI MNAYO!

    ReplyDelete
  3. Sasa kama jina la makonda ni jina mojawapo la ukoo wake,huku Gwaji akidanganya kwamba sijui kuna mtangazaji huko Tabora ndie alimpa jina,mnamfuatafuata nn?? Acheni mambo yasiyokuwa na msingi,kila mtu anaweza akabadili jina lake kwa kubatizwa ama kunuia na kidha kwenda mahakamani kulikana,haya mnaona mnavyoumbuka jina kumbe la babu yake,acheni mambo ya ajabu mtu amejiendeleza zake ame win maisha mnakazana lusimamia suala lisilokuwa na msingi badala ya kuangalia madhara ya dawa za kulevya ktk jamii..Makonda chapa kazi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bila Gwajima tungeyajuaje? Gwajima kasema jina la Paul Christian ndiyo kapewa cheti cha mtu mwingine..sio jina la Makonda...

      Delete
  4. Si kawaida sana mtu kwenda nyumba uliyowahi kulelewa na kuishia nje tu, lazima kuna sababu za kimsingi ambazo , naamini, yeye mwenyewe Makonda na pengine hata hao walezi wake wanazijua. Hivyo tuwaachie wao wenyewe, ni mambo ya kifamilia zaidi. Hata huko kumfukuza nyumbani kwao kwa kosa tu la mtoto kuchezea bunduki na kuleta hayo madhara, inatosha kupambanua hatima ya uhusiano kati ya Paul na hao walezi wake. Inawezekana hilo limechangia gap kati yao na lack of confidence. Labda Paul ana ujasiri zaidi wa kuwa approach vijana wenzie, pengine hata tangia akiwa bado analelewa. Pengine bado anawaogopa maana hawakusema walimfukuzaje na kwa kutumia maneno gani. natisha kwa wenye kupambnua kubaini uhusiano

    ReplyDelete
  5. MTAMSEMA-MCHANA-USIKU-MTALALA-YUPO-GADO!!

    ReplyDelete
  6. Alipotaja watu juu ya madawa kwa kuwaonea ndio nao wakaanza kumpekua uelewa na uweledi wake. Unapojifanya kupigana vita ya madawa kwa kuchanganya na visa binafsi unakaribisha reaction za kisasi au za kijinga vilevile. Ndio maana Daudi bashite aliibuliwa.

    ReplyDelete
  7. Pole kaka yangu Makonda,ziba masikio jembe letu.Mungu yuko pamoja na wewe ni wapwani bunju.Nakupenda makonda mungu akupe nguvu kwenye kipindi hiki kigumuu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Siku zote Mungu yupo na haki na wala si zaidi ya hapo..

      Delete
  8. BIG UP MACO N MAGU..MAY GOD BLESSING U ALL...

    ReplyDelete
  9. Double standard

    ReplyDelete

Top Post Ad