Nahitaji Ushauri, Mke Amebadilika Sana Tangu Mimi Niondoke..

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wadau hamjambo,

Naomba msaada, niko South Africa since last week, niliondoka Tz mpaka South Africa baada ya kupata mchongo kwa rafiki yangu ambaye alinitafutia mchongo wa kazi.

Namshukuru Mungu nilifika salama na maisha yanaendelea vyema kabisa.
suala kubwa lililopo ni kuhusu wife wangu, kipindi naondoka nilimshirikisha lakini alionekana kuwa na hasira sana juu ya uamuzi wangu wakuja South,

Nilijaribu sana kumsihi yakuwa nakuja kuangalia namna mambo au upepo ulivyo kisha nitageuza lakini alishindwa kunielewepa kabisa na kuwa mtu mwenye hasira kiasi ambacho hata unyumba alininyima.

Nikafikiri sana namna gani yakufanya, sikuona namna, maana nilikuwa tayari nishakatiwa ticket ya kuja na kurudi(Go and Return) yaani kama mambo yakiwa mabaya niko huru kurudi. Basi kiukweli nilichukua uamuzi mgumu nikafwatilia kila kitu na safari ikaiva yakuja South, nikaondoka na kufika salama.

Lakini kabla sijaondoka wife alinitumia sms na kuniambia nisimshirikishe lolote wala kumpigia wala kuhangaika na yeye.

Sasa tangu nimefika nimejaribu kumtumia sms, kutaka kujua hali ya maendeleo na nilimwomba hata akaunt ya bank ili nimtumie pesa kwa ajili ya matumizi, lakini wadau huyu mwanamke alinitukana na kunitumia sms za ajabu sana, oooh, wewe mwanaume gani, tena kwa taarifa yako nimeshapata baba wa mtoto na maneno mengine mengi ya ajabu.

Kweli najisikia vibaya sana na majuto kuwa na mwanamke mwenye hasira na asiye na kipimo cha maneno kwangu kwa heshima. Japo alinitukana vya kutosha lakini sijaacha kumtumia sms za kutaka kujua hali yake na mtoto, ila cha ajabu hajibu chochote.

Niko njiapanda, nishaurini nifanye nini, kwa wadau naombeni ushauri wenye hekima ili niuchukue maana niko mbali na ninahisi kuumia sana.

Please ushauri sio kejeli.

Thanks wadau.

Nawasilisha
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Panga safar urud nyumban kwanza ujue nn hasa kinamfanya awe vle au nenda naye south ikiwezekana nachoona anakupenda sana hataki ukae mbal nae ko jarbu kurud na angalia kama unaeza kwenda nae mchukue kama haiwezekan jaribu kumweka sawa hata kuwaeleza wazaz wake sanasana waongee nae

    ReplyDelete

Top Post Ad