Onyo kwa Bunge Dhidi ya Adhabu kwa Makonda...!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Ni hakika kwa100% Daud Albert Bashite alimaarufu Paul C. Makonda amekiri tuhuma zote mbele ya Kamati ya Bunge leo,

Kinachosubiriwa ni maoni ya kamati hiyo kwenda kwenye Bunge ambapo taarifa na maoni hayo vitasomwa Bunge linaloanza wiki ijayo 04/04/2017.

Mimi kama raia mwenye haki na wajibu kwa taifa langu, nikitambua haki yangu kwamba Bunge ni chombo changu cha uwakilishi, Natoa onyo kwa Kamati husika na Bunge pia, Ole wenu mje na hadithi ya kwamba MMEMSAMEHE.

Narudia ole wenu, Ole wenu, ole wenu kabisa..... Sisi wananchi tuna kesi nzito sana na huyu mtu nje ya yeye kutudharau na kutudhihaki kupitia bunge letu ambalo nyinyi tumewatuma mtuwakilishe...

Nataka mtambue kila mnachofanya hamfanyi kwaniaba yenu, bali kwaniaba yetu, Hivyo sisi tuliowatuma tayari tulishamhukumu na kufunga file lake.

Ole wenu mbadilishe maamuzi ya umma, Sisi ndio wenye mamlaka ya mwisho katika nchi hii, sio rais, sio jaji, sio spika, bali sisi tukisema na kuamua mbinguni na duniani tumeamua.... Hii ni kwamjibu wa katiba ya 1977 na ile inayopendekezwa ya Warioba na hata ile ya Marehemu Sitta bado hazikutung'anya mamlaka yetu.

Ukisikia kwamba mamlaka yote yanatoka kwa Mungu haimaanishi Mungu wa ulaya au asia, Mungu ni sisi Watanzania..
Sisi tukisema ni Mungu amesema!

Ole wenu wabunge!!!!!

Na Yerico Nyerere

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Usiseme watanzania,sio wote tupo side moja. Mi nipo side ya Makonda na nahitaji aendelee kutuondelea mateja barabarani. Nadhani hauna ndugu aliyeathirika I wish ungeona jinsi gani inauma kumuona Mdogo wako ni drug addicted (u just don't know how it pains). So stop saying kuwa watanzania wote tunataka makonda awe punished in anyways. Nonsense

    ReplyDelete
  2. Zitto, waxha kuzungumza utumbo mmimi simo..!!Makonda no Jasiru na Shupavu. Vita aliyo ianzisha maadui mko wengi. Na mungi anasimama nae hata Magu na sisi wote tunalitambua huko .Maoni haki hatana Mantiji zaidi ya chuki na. ..

    ReplyDelete
  3. UMEKOSEMA MUNGU SIO WATU.MUNGU MTAKATIFU AMEKUUMBA WEWE NA VYOTE DUNIANI.UKISEMA WEWE HAKUSEMA MUNGU.AKISEMA MUNGU HUKUSEMA WEWE.JARIBU KUSEMA MVUA INYESHE NYUMBANI KWAKO TU KAMA WEWE MUNGU.

    ReplyDelete
  4. WAUZA SEMBE UTAWAJUA TU.MUNGU ATAWAANGAMIZA KWA KELELE ZENU KWA MAKONDA.

    ReplyDelete
  5. Hmmm!
    It seems huyunjamaa hata media zikikubaliana kutomtaja bado anamake news.

    ReplyDelete
  6. Kweli nimeamini kuwa watanzania wengi waliishi kwa biashara hii ya madawa ya kulevya na ni watu wakubwa kabisa sasa wanaokoteza makosa ya RC Makonda ili tu aonekane si kitu. Mungu wetu mwenye haki atampigania Makonda hadi maadui wake wote mtashangaa. Mungu endelea kumjalia ujasiri RC Makonda. MUNGU IBARIKI TANZANIA, Mbariki RAIS wetu, Mbariki mkuu wa mkoa wa Dar

    ReplyDelete

Top Post Ad