15 Mar 2017

PolePole - Msiwe na Haraka Makonda Atashughulikiwa Kama Wanavyoshughulikiwa Wengine...!!!


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema taratibu zitafuatwa kuwawajibisha viongozi wake na wa serikali wanaokabiliwa na tuhuma na madai mbalimbali.

Polepole amesema hayo jana katika Makala ya Kinagaubaga, kipindi kinachorushwa na Idhaa ya Kiswahili ya Deutschen Welle(DW) baada ya kuulizwa swali kuhusu chama hicho kulea utovu wa nidhamu wa makada wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti wanaotuhumiwa kulidhalilisha Bunge na chombo hicho kwa kauli moja kutaka wajieleze.

Akijibu swali hilo Polepole alisema, "Ninyi hamkujua kama tutawachukulia watu juzi, Serikali ina utaratibu wake bunge lina utaratibu wake na chama kina utaratibu wake. Tunao utaratibu tunafuata, wananchi wawe na subira"

"Wananchi wawe na subira, ninafahamu wananchi wana subira sana, wasubiri mamlaka za viongozi, hawa wote waliokosea, mchakato wa haki ufanyike na hatimaye tutaona matunda yake."


Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Share:
Weka Maoni yako Hapa

4 comments:

 1. Chondechonde,msimnyazishe wala kumsinzisha kuhusu madawa ya kulevya,
  hiyo dhambi itawatafuna na nyie wote.

  ReplyDelete
 2. Kalidhalilisha bunge au wabunge wanajidhalilisha wenyewe???? Ukweli unauma sio....maana lile sio bunge bali ni 'kijiwe-nongwa'! masaa mawili mazima wanamjadili Makonda, kisa kasema wanasinzia bungeni, huku ni kweli wanasinzia na picha zipo! Baadae tunakuja kujuwa kumbe povu lote lile, wametumwa na Steve Nyerere wamwokoe Wema Sepetu hahahahah.....sijui kawalipa nini???
  Ni kweli kama alivyosema No.1 kwamba bungeni 'wanapiga porojo', bora lisirushwe LIVE.
  CCM wakimwadhibu Makonda wanamuonea, wakati ni kweli wabunge wanasinzia bungeni, akishtuka usingizini anaomba mwongozo. MNYONGE MNYONGENI, HAKI YAKE MPENI.

  ReplyDelete
 3. makonda endelea na kazi. super gluu masikio.. hawa wote wanafaidika kwa njia moja au nyingine na madawa

  ReplyDelete
 4. Kwani uongo bungeni si wanalala na kulifanya Bunge kuwa sehemu ya uwanja wa vita? Kwa hilo Makonda atahukumiwa bure, ningekuwa Makonda natafuta clip za wabunge wakiwa wamelala na kuzirusha TV watu wawaone.

  ReplyDelete


Popular Posts

Matangazo

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger