20 Apr 2017

NABII Afrika Kusini Aliyetabiri Tetemeko la Kagera Atabiri Kifo cha Kiongozi wa Upinzani Nchini..Adai Mwaka 2018 Utakuwa Mwaka Mbaya kwa Tanzania..!!!


Kiongozi wa Kanisa la Enlightened Christian Gathering (ECG) la Afrika Kusini, Nabii Shepher Bushiri amemtabiria ugonjwa hatari kiongozi wa upinzani wa Tanzania, akisema maombi pekee na imani yake ndio vitamnusuru asitokewe na “kitu kibaya”.

Nabii Bushiri pia amesema mwaka 2018 utakuwa mgumu kwa Tanzania kuliko wakati mwingine wowote, akishauri wananchi wafanye maombi kuiepusha nchi na hali hiyo.

Bushiri alisema hayo wakati wa ibada ya Sikukuu ya Pasaka iliyofanyika katika kanisa lake nchini Afrika Kusini na kurushwa moja kwa moja katika mitandao ya kijamii.

“Tanzania itapata shida ambayo haijawahi kuiona. Sisi kama kanisa, ni jukumu letu kuyaombea mataifa kwa sababu tumeitwa kwa ajili ya mataifa,” alisema Nabii Bushiri akiwa ameshika bendera ya Taifa ya Tanzania mkononi na shingoni akiwa amejifunga skafu yenye rangi za bendera hiyo.

“Tunaiombea Tanzania katika mwaka 2018, huruma za Mungu ziwe juu ya Tanzania kwa mwaka 2018. Tunaomba katika jina la Yesu. Tunaomba ulinzi.”

Wakati akiendelea na maombi hayo katika kanisa lililojaa waumini walioshika bendera za nchi zao, Bushiri aligeuzia maombi kwa ajili ya kiongozi huyo wa upinzani Tanzania.

“Tunamuombea kiongozi wa upinzani, kiongozi wa upinzani. Naona tatizo linaibuka kwenye ini lake. Lakini tunaomba huruma (ya Mungu) nazungumza kijasiri kadri ninavyoweza, kwa sababu najua (hili) linatoka kwa Bwana,” alisema nabii huyo. “Narudia hili. Nililizungumza miezi kadhaa iliyopita, (lakini) narudia kuhusu huyu mtu. Muda mfupi ujao ataanza kuzizima kama mtu anayesikia baridi. Lakini ni shambulizi hatari ambalo linahitaji maombi. Bila hivyo, kitu kibaya kitamtokea.

“Lakini mimi na wewe tunaweza kuzuia kama hata yeye ana imani. Lakini tatizo ni kwamba sioni imani kwake. Tunamuombea na tunaomba ulinzi. Inaweza isitokee sasa, lakini tunaomba ulinzi wa maisha yake.”

Nabii Bushiri ni mzaliwa wa Malawi, lakini anafanya huduma zake na biashara nchini Afrika Kusini ambako amejizolea waumini kutoka mataifa mbalimbali.

Bushiri aliwahi kutabiri kutokea kwa tetemeko la ardhi nchini Tanzania wakati alipotembelea Dar es Salaam Julai mwaka jana. “Nakumbuka mwezi uliopita, Mungu alinituma Tanzania kwenda kuzuia mauti. Nilikuwa nasali saa 1:00 asubuhi na nusu yake ikageuka kuwa damu,” alisema Bushiri katika mahubiri yake ya Julai 14, 2016 jijini Dar es Salaam.

“Nilimuuliza Mungu, nini maana yake. Na Mungu akaniambia ‘siku ya damu inakuja’. Nikasema hilo ni nini. Niliona watu wakifanya mambo yao na ghafla nikaona damu ardhini. Na Mungu akaniambia ‘iombee Tanzania’.

“Nilipokuwa nikiomba, nikaanza kutetemeka. Mwili wangu ulikuwa ukitetemeka. Na nikamuuliza Mungu, mtetemeko huu ni wa nini? Na Mungu akaniambia ‘hili ni tetemeko la ardhi. Si Dar es Salaam. Kutakuwa na tetemeko sehemu nyingine ya nchi.”

Katika ibada hiyo, Nabii Bushiri aliwataka waumini wake waiombee Tanzania kuiepusha na janga hilo.


Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Share:
Weka Maoni yako Hapa

4 comments:

 1. That is shirki... mungu pekee ndo mwenyekujua yajayo..

  ReplyDelete
 2. Watu wanaingilia uwezo wa MUNGU. Ni kujipachika unabii!!!!!

  ReplyDelete
 3. Ewe Baba wa Mbinguni. Wachukue waha wanaojiita Viongozi wa Kambi Rasmi ili uwapumzishe milele Kwa Damu ya Bwana aliye Hai. MTowe na Jitto na Kissu na bila kuwazahau Grop lao,uwachukue haraka uwape maisha ya milele kwako. Na Utuwachie JPJM wetu atutengenezee Nchi na adumishe Amani ya Milele TZ. Ameen

  ReplyDelete
 4. hahahahhaahah huyu mtabiri chizi wakati tetemeko la bukoba mbona hajagundua watu wamekufa mvua ya kahama vipi ye anajua yatayomkuta watu wengine bana mtihani tanzania ni nchi ya amani haitakuwa na chochote kibaya mungu ibariki tanzania na watu wake ameen

  ReplyDelete

Total Pageviews


Popular Posts

Matangazo

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger