21 Apr 2017

PAUL Makonda na Bongo Movie Mchawi Wenu Huyu Hapa...

Matatizo ya Bongo movies hayajaletwa na kuuzwa kwa filamu za nje nchini hili hata mtoto mdogo anafahamu. Yalianza kumea taratibu mpaka sasa ndio yamefikia kilele chake. Tunalaumu filamu za nje kutokana tu tu na tabia yetu watanzania ya kujificha nyuma ya ukweli. Nchini Korea kabla ya mwaka 2006 hali ya filamu zao ilikuwa dhofu lihali lakini hawakuchukua hatua ya kuzuia filamu za marekani bali walikaa chini na kumtafuta mchawi wakaweka mipango ya muda mrefu wakafanikiwa. 

Bongo movie mchawi wenu ni mambo makuu matano. 
1.Elimu, Mipango na Malengo (self awareness, planning and goals) 
2.Maudhui (contents) 
3.uzalishaji (production) 
4.Masoko (Marketing) 
5.Wasanii (actors &actress)

1. Elimu,Mipango na malengo
Ukifuatilia wasanii na directors wakubwa duniani waliofanikiwa sana kupitia filamu utagundua wana elimu kubwa sana hadi za vyuo vikuu vya sanaa. Bongo movies wamekosa elimu kabisa. Wanafanya mambo kienyeji enyeji tu. Cha kufanya Sasa hawawezi kurudi shule lakini wanaweza kutafuta watu waliosoma na has a wenzetu wazungu waliofanikiwa tayari wakawasaidia kufika wanapotaka hapa nazungumzia directors na the whole proctuction team. Iteni mkutano watafuteni kina Ernest Napoleon, Tafuteni wale directors wazungu wa Siri ya mtungi kaeni chini tafuteni njia ya kutoka. 

2. Maudhui hapa naomba niseme mnafeli sana. Story ndio moyo wa filamu. Tuna watunzi wazuri sana wa hadithi na riwaya nchini. Kina Hussein Tuwa, erick shigongo, Shaffih Adamu shaffi, na wengineo lakini sidhani kama kuna msanii au kampuni ya bongo iliwahi kuwafuata na kutaka kufanya kazi nao. Tunataka kuenda kienyeji enyeji. Utasikia Ray au JB anakwambia story nimetunga Mimi blah, blah, blah, tangu lini we ukawa writer?? Ndio maana tunapata story zile zile zinazoboa na kuchosha. 

3. Uzalishaji. Piga ua lazima kutumia gharama na muda na teknojia katika production kama unataka kufika mbali. Vifaa vya kisasa,teknolojia ya computer n.k . Bongo flavor walikubali na kutoka nje ya nchi kufanya production na watu wanaojua kazi.Nendeni nje ya nchi tafuteni producers wenye vifaa,elimu, na kujua kutumia teknolojia vizuri muwalete nchini tafuteni watunzi bora tumieni mazingira mazuri ya Tanzania tengenezeni vitu vizur mafanikio yatakuja. Siri ya mtungi ilifanyiwa production na wenzetu wazungu, itafuteni mfananishe na uchafu wenu wa part one na part two. 

4. Masoko. Naomba niwaambieni dunia ya sasa msanii huwezi tegemea CD na kufanikiwa inaonesha jinsi gani hamfikirii kabisa. Hivi ukizuia machinga kuuza filamu za nje? Utamzuai kuburn na kuduplicate copy ya hizo cd zako? 
Filamu sasa soko lake kubwa ni cable channels (kama Netflix) na Movie Theatre. kama we ni bongo movie unasoma hapa tafuta Netflix ni nini ujifunze. 
Mlivyokaa na mkuu wa mkoa nilitegemea mtamwomba Bongo movie Theatres. Imagine kuna bongo Movies Theatres majiji tote makubwa nchini pamoja na miji mikubwa nchi jirani kama Nairobi, Kampala, Kigali n.k Then inaoneshwa filamu ya bongo yenye viwango vya kimataifa inaoneshwa huko. Mmeshajiuliza mtapiga mkwacha kiasi gani? Niliwahi kuwa na mzungu mmoja kila Siku anataka nimpeleke Movie Theatre ya filamu za kibongo lakini hamna. Kiswahili ni fursa kubwa ya Bongo movie kukitumia kupiga hela. 

5. Wasanii. 
Wasanii wa nchi hii ni tatizo kubwa na wana njaa iliyopitiliza. Mnafuata nini kwenye siasa nyie, hivi mnajua mna mashabiki wa vyama vyote. Unapovaa nguo za chama Fulani unajiulizaga umepoteza wateja milioni ngapi kutoka chama kingine?. Umewahi kumuona denzel Washington au will Smith amevaa nguo za chama? Acheni njaa. 
Wewe kama msanii mwonekano wako ndio office yako unajitunza vipi. Mnakula mnajisahau mnanenepeana hovyo. Unaangalia bongo movie ni vitambi tuu vimejaa alafu mnalalamika movie za nje zinawaharibia soko. Jitambueni.

By Time Treveller

Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Share:
Weka Maoni yako Hapa

1 comment:

  1. elimu ndio kila kitu nyie kweli mnachekesha munakwenda kwa mtu aliepata zero zero awasaidie vipi haa haaa he jamani bongo movie au na nyie muliokwenda ndio kama mulie muendea bashite.
    amkeni kuweni makini munatia aibu Tanzania wasani wachache kwa hesabu ambao wanajitambua kingereza kime wapiga chenga hata kiswahili munashindwa kutuletea film nzuri jamani halafu rti munajiita celebrity from where kaaeni tu na huyo muuza sura

    ReplyDelete

Total Pageviews


Popular Posts

Matangazo

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger