RAY Kigosi Afunguka Mambo Mazito Kuhusu Marehemu Kanumba Kuhusika na na Uchawi wa Freemason..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Msanii wa filamu nchini Ray Kigosi amefunguka na kusema kuwa baadhi wa Watanzania ni wanafiki na wamekuwa wakikatisha tamaa watu katika mambo yao kutokana na unafiki wao.

Ray Kigosi amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instgram na kusema kutokana na unafiki huo wa baadhi ya watu ulimfanya mpaka marehemu Kanumba kuvunjwa moyo katika kazi yake.

==>Ray Kigosi ameandika;
1. Kanumba alipoanza kuona mwanga wa kufanikiwa bila kujali juhudi zake kuna watu walimuita Freemanson, Mara anatumia nguvu za Giza. that is to say films zake hazikuwa nzuri but ziliuza sababu ya nguvu za Freemanson na nguvu za giza!!

2. Kanumba alipoenda Big Brother alipondwa Sana na kuitwa bogus kwa Madai hajui kiingereza, Ni watanzania Hawa Hawa walibebea bango hili huku baadhi ya waandishi uchwara wakieneza ujinga huu bila kujali juhudi zake. But Leo wanamsifia hakuna Kama Kanumba!

3. Kuna wakati Kanumba alionekana wazi kuvunjwa moyo na kukatishwa tamaa kwa kuonekana juhudi zake si kitu. But Alisema maneno machache Kuwa mtanikumbuka kama si Leo basi Ni Kesho.
And alichosema kimetimia, wale wale waliokuwa wakisema Ni Freemanson bila hata kujali juhudi zake kwenye game Leo ndio kwa unafiki wanasema hakuna Kama Kanumba !….. HAO NDIO BINADAMU NA TABIA ZAO
Je Kanumba kaondoka na Bongo Movie yake ya Freemanson ? Kama wengine mnavyodhani industry Ni Mtu sio system !

4. Diamond Platnumz nae baada ya kuona Njia ya mafanikio kuna watanzania, wasanii wenzake na hata baadhi ya wanahabari wanasema Ni Freemanson, wengine wanaonyesha chuki ya wazi kwake. Wanasema Hana muziki mzuri, Mara Ni Kiki tu ambazo hata Kanumba alikuwa akiripotiwa magazetini na kina Wema.

Hawaoni juhudi na thamani ya Diamond sasa ! Hatuombi baya limpate Diamond ili kudhibitisha tabia na unafiki wa binadamu. But HAO NDIO BINADAMU siku zote hawana Jema unafiki ni sehemu ya Maisha.

5. kila siku Ni kuzua hii na kile, Mara ooh Diamond Ni mchawi, kasema mleteni huyo mganga wangu mkashindwa kumleta, akajitokeza mganga fake sijui na Madai juu Kuwa Diamond atashuka kimuziki kwa sababu ananipuuza niliyempa nyota, Diamond akasema sawa namtegemea Mungu. Miaka 4 sasa tangu yaliyoitwa ya mganga Diamond hashuki ndio anazidi kupaa. HAO NDIO BINADAMU kusema lolote Ni haki Yao.

Kazi za Kanumba sasa zinapewa thamani na ubora uliovuka mipaka na viwango ambao hakupewa kipindi yupo hai ! HAO NDIO BINADAMU na tabia zao. Ni tabia tu ya baadhi ya watu kubebea mabango mabaya ya Mtu au uzushi na kuacha mazuri yake then baadaye wakishikwa Uchawi wanageuza walichoamini Ni nyeusi kiwe nye.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Unatafuta kurudi midomoni mwa watu kwa mgongo wa kanumba, umeshapotea kwe game, tumia huo muda kurekebisha pale unapoona hapajakaa sawa, mwachen kanumba wa watu apumzike. Kiukweli movie zenu nyingi hazivutii walau akicheza Gabo, mboto, slim, riyama na mama grace mapunda au bi mwenda kidogo wanajitahidi kuweka uhalisia kwenye wanachokiigiza. Achen maneno kubalin kubadilika pokeen maoni ya wananchi mjue watu wanataka nin toka kwenu. Binafsi ukinikuta naangalia bongo movie jua natazama Huba, muda mwingi nipo kwe tamthilia za wahindi na wafilipino. Polen bongo movie acheni ngenga weken uhalisia

    ReplyDelete

Top Post Ad