SERIKALI Yamfukuza Bosi wa UN, Aondolewa Nchini Ndani ya Saa 24, Chanzo Chadaiwa ni Kuhoji Ushindi wa CCM ZNZ na Kumsaidia Maalim Seif Kuishitaki Tanzania Kimataifa.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Serikali imemwondoa nchini Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo.

Mkurugenzi huyo raia wa Gambia, aliyeletwa nchini na Umoja wa Mataifa (UN) Agosti 2015, aliondolewa wiki iliyopita ndani ya saa 24 kwa agizo la Serikali, huku akiwa chini ya ulinzi. Hadi sasa haijaelezwa sababu za kuondolewa 

Mtanzania ilipomfuata Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mindi Kasiga ili kupata ufafanuzi wa kina wa tukio hilo, akijibu kwa kifupi kuwa anayepaswa kuzungumzia hilo ni UNDP na si Serikali 

"Ninakuomba watafute UNDP wenyewe ndio wanaweza kuzungumzia hilo kwa sasa", alisema Mindi 

Ulipofuatwa uongozi wa UNDP, Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika hilo la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu, alithibitisha kuondolewa nchini kwa mkurugenzi huyo 

"Ni kweli mkurugenzi wetu ameondolewa nchini ila kwa maelezo zaidi wasiliana na upande wa Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa au mtafute Mindi (Msemaji wa Wizara)", alisema Hoyce 

Mtanzania lilipomfutafuta tena Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mindi ili kuzungumzia sababu za kuondolewa kwa kiongozi huyo, hakuwa tayari kuzungumza suala hilo ila alithibitisha kuondolewa kwake 

"Ni kweli (Mkurugenzi wa UNDP) ameondolewa nchini, ila sasa sababu mimi binafsi sijazijua, anayetakiwa kuzieleza ni Katibu Mkuu, hivyo kama atasema tutaueleza umma", alisema Mindi 

Alipotafutwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Suzan Kolimba kwa simu, alisema kwa sasa hajui lolote kuhusu suala hilo. 

"Sina taarifa hizo, nipo bungeni labda kwanza nifanye 'follow up' kisha ndiyo nikwambie, au nitamwagiza mkurugenzi atakupatia taarifa tu usijali", alisema Dk. Suzan 

Akizungumzia kuondolewa kwa kiongozi huyo, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Aziz Mlima, alisema kuwa kulitokana na kuibuka kwa mgogoro kati yake na wafanyakazi wa UNDP waliopo nchini 

Dk. Mlima alisema baada ya kuibuka kwa mgogoro huo, Serikali iliamua kuandika barua Umoja wa Mataifa ikitaka kuondolewa kwa mkurugenzi huyo. 

"Unajua unapokuwa kiongozi kama huyo ana kinga ya ubalozi, ni lazima ufuate utaratibu na si vinginevyo, hivyo baada ya tukio hilo tuliandika barua kati ya Aprili 6 au 7 na kuomba kuondolewa kwa kiongozi huyo. 

"Na kikubwa unapokuja katika nchi yetu ni lazima ushirikiane na Serikali iliyopo na si vinginevyo na kwenda kinyume ni sawa na ukwamishaji wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2020. Na UNDP ni mbin mkubwa wa maendeleo kwa nchi yetu, ila kama unakuja tofauti na malengo na kazi za UNDP, huku ni kuleta mgogoro ", alisema Dk. Malima 

Alisema mara nyingi Serikali imekuwa ikitoa heshima zote kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwamo UNDP, lakini pindi inapobainika yanakwenda kinyume na malengo ya kazi, katu Serikali haiwezi kuruhusu hali hiyo.

TAARIFA ZA NDANI 

Chanzo cha kuaminika kiliiambia Mtanzania kuwa sababu ya kuondolewa kwa mkurugenzi huyo ni pamoja na hatua yake ya kuingilia baadhi ya mambo katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25, mwaka 2015 pamoja na ule wa marudio wa Machi 20, mwaka jana.

Hatua hiyo inaelezwa kutowafurahisha baadhi ya viongozi wa Serikali 

"Kuondolewa kwa mkurugenzi huyo kumechangiwa pia na alichoandika katika ripoti yake kwenye Umoja wa Mataifa (UN) kuhusu utata wa uchaguzi huo ambao Maalim Seif Sharif Hamad, aliulalamikia na kudai yeye ndiye mshindi. 

"Si hilo tu, pia inaelezwa kuwa yapo baadhi ya matukio ambayo anatajwa nayo moja kwa moja ikiwemo kuwasikiliza baadhi ya viongozi walioshiriki uchaguzi na kushindwa, ikiwemo kuwapa mbinu za namna ya kuwasilisha malalamiko yao kwa vyombo vya kimataifa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Non grants person. Hakuletwa na Unpd kuingilia siasa. Akitaka siasa aakkajiandikishe na achukue. Fomu huko Gambia na siyo newyuki. Amepoteza dira la mwajiri wake UN NA LAKE MWENYEWE WALA YA sefu shariff wakutane what sup na twitter kama SI esi hiimeli.amekosea namba mama mwe

    ReplyDelete

Top Post Ad