A to Z ya Video Chafu ya Gigy Money na Wakili Msando...Msando Adai Gigy Amelipiza Kisasi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Aibu! Siri nzito imevuja baada ya video chafu iliyomhusisha wakili maarufu hapa nchini ambaye pia aliwahi kusimamia kesi ya Wema Sepetu, Albert Msando na muuza sura katika video za wasanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’.

Video hiyo inamuonyesha Msando akimshikashika sehemu nyeti msichana huyo ambaye naye anajibu kwa kumkatikia mauno mwanasheria huyo msomi. Wakati wadau mbalimbali wakimlaumu Msando kwa kile walichosema amejishushia heshima, Risasi Mchanganyiko limebaini kuwa ishu hiyo haikutokea kwa bahati mbaya, bali ni kisasi kilichopangiliwa kwa ustadi.

MWANZO WA MCHEZO

Gigy Money alikuwa katika ziara ya kimuziki katika Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro akiwa na rafiki yake mmoja ambaye jina lake halikufahamika, aliyekuwa akifanya mawasiliano na mwanasheria huyo maarufu nchini, ambaye wakati huo alikuwa Arusha.

HUYU HAPA GIGY AKIMWAGA MBOGA…

Akizungumza baada ya video hiyo kuvuja, Gigy alisema wiki iliyopita alikuwa na shoo maeneo ya Boma, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ambako akiwa huko alipata mwaliko kutoka kwa Msando wa kwenda kumtembelea katika klabu yake iitwayo The Don, iliyopo Arusha.

“Kweli Msando nilikuwa sijawahi kuonana naye live, ila aliposikia nipo Hai akanipa mwaliko, nikamwambia siwezi kwenda kwa kuwa nilikuwa bize na shoo, pia sikuona umuhimu sana wa kumuona maana sicho kilichonipeleka. “Baada ya kusema atanitumia usafiri, nikakubali, nilipomaliza kazi alikuja na gari akiwa na watu wanne, wanaume wawili na wanawake wawili, tulifika Arusha tukaenda club, nikalewa sana na baada ya hapo wakanipa tena lifti kwenye gari yao kwenda hotelini.

“Tukiwa kwenye gari huku nimelewa, nilisikia Msando akimwambia mmoja wa wale watu aturekodi nami sikuelewa ana maana gani, wakanishusha nikaenda kulala peke yangu, sijalala na mtu yeyote, kesho yake nikaiona kwenye mitandao, kiukweli kitendo hicho hakijanifurahisha hata kidogo, kimeniudhi mno maana kimenidhalilisha,” alisema Gigy.

MSIKIE MSANDO SASA

Risasi Mchanganyiko lilijaribu mara kadhaa kumpigia simu yake ya mkononi bila kupokelewa, lakini baada ya kutumiwa ujumbe mfupi wa simu, likijitambulisha na kuomba kupata ufafanuzi kuhusu video iliyopo mtandaoni, Msando alipiga simu na kuzungumza.

Risasi: Mambo vipi kaka!

Msando: Safi aisee.

Risasi: Pole kwa kilichotokea mzee.

Msando: Aaah ndiyo imeshatokea tena haina jinsi.

Risasi: Kwani ilikuwaje kaka?

Msando: Aaah, unajua kilichotokea ni kama huyu dada amenilipizia hivi!

Risasi: Kivipi? Msando: Si unajua huyu dada aliwahi kusema kuwa hakumbuki ame-date na watu wangapi? Sasa mimi kuna siku nilipost (kuandika katika mitandao ya kijamii) nikishangaa kama kwa miaka miwili tu ameshawasahau, basi kuna tabu.

Sasa najua kuanzia pale akawa na hasira na mimi.

Risasi: Kwani mnafahamiana kabla ya leo?

Msando: Sijawahi kuwa na mawasiliano naye hata mara moja.

Risasi: Khaa, sasa kama hamjawahi kuwasiliana ilikuwaje ikawa kama vile ilivyokuwa?

Msando: Mimi nilikuwa nawasiliana na dada mmoja ambaye alikuwa anatumia simu ya Gigy, aliniambia wanataka sana kuja kupaona klabu kwangu, nikaona isiwe tabu, nikawakaribisha.

Risasi: Kwani wewe una klabu?

Msando: Ndiyo, inaitwa The Don, ipo Njiro.

Risasi: Aisee, safi kaka, uko vizuri. Enhee, ikawaje sasa?

Msando: Basi wakaja ile usiku sana, tukawa pamoja tunapata mambo, hadi kunakaribia kucha tukaondoka.
Risasi: Sasa ile video ilirekodiwa wapi?

Msando: Ndani ya gari wakati tunarudi, aliyekuwa anatupiga picha ni rafiki yake. Risasi: Hukuelewa kama unarekodiwa au uliruhusu jambo hilo lifanyike?

Msando: Aaah, si unajua tena mambo yale, sikufikiria chochote aisee.

Risasi: Lakini Gigy analaumu kuwa ni wewe ndiye uliyeingiza mtandaoni ile video. Msando: No, ni namba ya Gigy ndiyo iliyoingiza mtandaoni.

Risasi: Kwa hiyo unafikiria kumchukulia hatua za kisheria Gigy? Msando: Hapana, nina vitu vingi sana vikubwa vya kushughulika navyo kuliko kushughulika na mtu kama Gigy, ninamuacha tu! Risasi: Dah, na vipi mke wako ameshaiona?

Msando: Yes ameiona. Risasi: Vipi mapokeo yake?

Msando: Mke wangu ni sapota wangu namba moja, anajua baada ya pale hakuna kilichoendelea, kwa hiyo iko vizuri. Mimi nina mke, watoto na ndugu zangu na wa mke wangu pia, kwa hiyo hili jambo liko vizuri tu kwa upande wangu.

Risasi: Sawa, lakini una wateja wako na watu wengine wanaokuheshimu, unawaambia nini kwa hili?

Msando: Nimeandika kwenye ukurasa wangu wa Instagram, unaweza kupitia.

Risasi: Asante, nitakutafuta kukiwa na ishu nyingine broo.

Msando: Asante karibu. Katika akaunti yake ya Instagram, Msando aliandika maneno haya kwa wateja wake, marafiki na watu wake
wa karibu. Nikikaa kimya nitakuwa mnafiki. Nimekosea. Kilichotokea hakikupaswa kutokea. I will be a man enough and say sorry kwa wote ambao nimewakwaza na kuwaangusha. Am so sorry. But the beauty of all this is we are all human. Kuna watu ambao wamekuwa wepesi kuhukumu. Siwalaumu. Ni sawa, ni haki yao. I made a stupid mistake. I take full responsibility. Mwisho wa siku maisha lazima yaendelee. It could have been worse. And to all those who took time to text I appreciate. Thats friendship. Kulikuwa na maneno katika baadhi ya mitandao, wakitaka Chama Cha Wanasheria Tanzania (TLS) kumchukulia hatua Msando, kwani amekidhalilisha. Lakini Risasi Mchanganyiko lilipofanya mawasiliano na rais wa taasisi hiyo, Tundu Lisu alisema;

TUNDU LISU APIGILIA MSUMARI

“Msando ni mwanachama wetu, lakini sisi kama chama hatuwezi kumchukulia hatua yoyote, angekuwa amefanya kosa hilo akiwa katika kazi zake za kisheria, hapo sawa, lakini hili ni jambo binafsi. Wakili hazuiwi kunywa pombe, hazuiwi kuchukua malaya, kwa sababu hayo ni mambo yake, ni juu ya kanisa lake au mke wake kushughulika naye, siyo sisi.”

AJIUZULU

Wakati tukienda mitamboni, Wakili Msando alitoa taarifa ya kujiuzulu nafasi yake kama Mshauri Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo, ambayo aliielekeza kwa kiongozi wake mkuu, Mbunge wa
Kigoma Mjini, Zitto Kabwe. “Napenda kuchukua nafasi hii kukujulisha uamuzi wangu wa kujiuzulu nafasi yangu kama Mshauri Mkuu wa Chama.

Uamuzi huu ni kutimiza hitaji langu la kuishi kama mfano kwa jamii inayonizunguka. Kama kiongozi nastahili kuwajibika kutokana na video clip iliyorekodiwa na kusambazwa. Ni wajibu wangu kwa chama changu na nchi yangu kuwajibika kama kiongozi. “Nitaendelea kuwa mwanachama mtiifu nikishirikiana nawe kujenga chama na kuhakikisha nchi yetu inaendelea mbele.

Nakushukuru kwa kuniamini kwa kipindi chote tulichofanya kazi pamoja,” alisema Msando katika taarifa yake. Zitto hakuchelewa kumjibu mshauri huyo, akisema amepokea barua yake ya kuomba kujiuzulu nafasi yake na yeye amekubali. “Ndugu Albert Msando amekuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika chama katika nafasi mbalimbali alizoshika.

Chama kinamshukuru kwa moyo wake wa kizalendo na mchango alioutoa. Ni matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi katika ujenzi wa chama kwa kadiri atakavyoweza na atakapohitajika kama mwanachama. “Nikiwa kiongozi wa Chama nimekubali kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika kujisahihisha kwake. Ndugu Msando Albert ameomba msamaha kwa jamii kwa uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia kupita katika mitihani iliyomkumba,” ilimalizia taarifa hiyo ya Zitto jana.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad