Baada ya Rais Magufuli Kufichua Ufisadi Mkubwa wa Serikali ya Awamu ya Nne na Tatu Jana..Afande Awataka Mkapa na Kikwete Kutubu..!!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Msanii wa muziki wa bongo fleva, Afande Sele amefunguka na kusema kama angekuwa ni mmoja kati ya Rais wa awamu ya tatu au awamu ya nne basi angekaa kimya na kujifungia ndani huku akitubu na kuwaomba radhi wananchi kwa mambo waliofanya.

Afande Sele ambaye pia ni mwanasiasa aliyegombea ubunge jimbo la Morogoro Mjini kupitia ACT Wazalendo, amesema hayo siku moja baada ya Rais John Pombe Magufuli kupokea ripoti ya uchunguzi wa madini ambayo imeonyesha kulikuwa na wizi mkubwa jambo lililopelekea Rais kumtengua Prof. Muhongo katika nafasi yake ya Waziri wa Nishati na Madini.

"Baada ya kupata matokeo ya taarifa ya tume iliyoundwa na Rais Magufuli kuhusu usitishwaji wa kusafirisha mchanga wa madini kwenda nje ya nchi. Nimechoka mwili na akili kwa jinsi kama taifa lenye mamilioni ya watu masikini sana tulivyokuwa tunapoteza mabilioni ya dolla kikatili kabisa kwa makusudi ya watanzania wenzetu wachache tena wale tuliokua tumewapa dhamana kuu za kutuongoza." alisema Afande Sele

Afande Sele alizidi kusisitiza kuwa viongozi hao wanapaswa kuomba radhi kwa wananchi kwa madudu ambayo wamefanya kipindi cha utawala wao 

"Kwa sababu uso umeumbwa na haya na kwa sababu mimi siyo mwanahizaya. Laiti kama mimi ningekua ni mmoja kati ya watu hawa daima ningefunga mdomo wangu, ningejifungia ndani kwangu, ningetubu kwa Mungu wangu, ningewaomba msamaha wananchi wenzangu kwani wametia aibu wanapaswa kutubu" alisema Afande Sele 
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wengine si viongozi Bali mradi viongozi. Kama hao wawili waliopita. Alafu hawana hata miyoyo ya huruma wala mishipa ya haya. Sasa watu wa Aina hii. Binadam tutawaitaje kama si mabaradhuli hawa

    ReplyDelete

Top Post Ad