Kocha Agoma Kung'atuka Mbao FC

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kocha wa Mbao FC, Ettiene Ndayiragije raia wa Burundi, amesema mkataba wake unamzuia kuanza kufikiria kujiunga na timu nyingine ambazo zinatajwa kumuwania.

Ndayiragije ambaye aliwahi kuinoa Vital’O ya nchini kwao, ameyasema hayo huku kukiwa na tetesi kwamba anatakiwa kwenda kuchukua mikoba ya Mmalawi, Kinnah Phiri ya kukinoa kikosi cha Mbeya City.

Mrundi huyo amesema kuwa, kutokana na mkataba wake alioingia na Mbao, unamnyima nafasi ya kuanza kupigia hesabu timu nyingine.

“Si kweli kama nataka kwenda Mbeya City, mimi ni kocha wa Mbao na watu wanatakiwa kulitambua hilo kwamba sina mpango wa kuondoka sasa hivi na mkataba wangu na Mbao unanizuia kuanza kufikiria kujiunga na timu nyingine, inawezekana ipo timu inayonihitaji lakini binafsi sina taarifa hizo na sijafanya mazungumzo na timu nyingine,” amesema Ndayiragije.

Kocha huyo alisaini mkataba wa mwaka mmoja ambao unaisha hivi karibuni, lakini mwenyewe amesisitiza kuna makubaliano ambayo aliingia na mabosi wake. Makubaliano hayo alidai ni siri yao.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad