Ruge Ajibu Baada ya Kuambiwa ni Makonda Kuwa na Mtunga Nyimbo za Mapenzi na Ngonjera

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mkurugenzi na mzalishaji wa vipindi waClouds Media Group, Ruge Mutahaba, ameijibu kauli iliyotolewa na Mkuu wa mkoa wa Dar Dar es salaam, Paul Makonda ya kuwa yeye ni muongo, na anafaa tu kuwa muandishi wa mashairi na nyimbo za mapenzi na ngonjera.


Ruge ametoa kauli hiyo leo katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na kituo hicho, ambapo walikuwa na kipindi cha ‘SHUKRANI’ kwa wasikilizaji wao na watu waliowahi kuwasaidia kupata misaada.


“Kila mtu ana mtazamo wake, na huwezi kulazimisha mtazamo wa mtu ubadilike. Inasikitisha sana kuona mtu anayesambaza haya mambo ni bosi wangu, Bosi wa mkoa wetu. Yeye akipiga mhuri kitu ndio imekaa hiyo, Yeye ana nguvu zote,” amesema Ruge.


“Sasa akisema hivyo mimi ni tapeli anataka kila mtu Dar es Salaam anione hivyo. Mimi sina nguvu kwa hiyo nachagua kubaki kwenye ninacho kiamini. Tangu mwanzo nilisema mimi nataka haya mambo yaishe, cha kusikitisha huyu mtu ni kiongozi lakini anashindwa kumaliza jambo hili kwa busara na anataka kuliendeleza.


“Kuna mambo hapa yanajaribu kutengenezwa. Watu wanajaribu kutusukuma turudi kwenye mjadala ambao tulishaumaliza. Mimi ni mtu mzima , na busara inaniambia watu wazima hatuna haja ya kurudi kwenye majibizano ambayo kwangu yaliisha siku nyingi “alieleza Ruge.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ruge umeongea na kumjibu vizuri sana hiyo nimeipenda sana!Short and clear with very strong points ndani yake.Kwa hili umeona mbali sana! Ubarikiwe.

    ReplyDelete
  2. Things to be settled amicably and if one side decided to cool down other part should adhered ...mijadala hii haina tija.

    ReplyDelete
  3. Things to be settled amicably and if one side decided to cool down other part should adhered ...mijadala hii haina tija.

    ReplyDelete

Top Post Ad