17 May 2017

UTATA na Historia ya Salum bin Almasi Aliyeuawa Kurasini Akituhumiwa ni Jambazi..!!!


Salum Mohamed Almasi alizaliwa mwaka 1989 ni mjukuu wa sheikh Muhammad bin Abdurrahman Ashadhuly. Alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Kivinje iliyopo Kilwa Kivinje darasa la kwanza mpaka la nne akahamia Masasi kwa mjomba wake Dr. Tondwa na kuendelea hadi kumalizia elimu ya msingi shule ya msingi Mkomaindo iliyo Masasi akaendelea na elimu ya sekondari Masasi day kidato cha kwanza hadi cha nne akachaguliwa kidato cha tano Ndanda high school na akahamia Tambaza high school kidato cha 6 mchepuo wa PGM. Aka dahiliwa katika chuo cha Saint Joseph college of engeering campus ya Songea course ya computer science lakini alishindwa kuendelea kwakukosa mkopo na kua ametoka katika familia isokua na uwezo wa kifedha akakaa nyumbani. Mwaka jana alijiunga na university of Dar es salaam computing centre UCC akisoma course ya ICT in networking ngazi ya stashahada mpaka unamfika umauti alikua ni mwanachuo mwaka wa pili UCC huku akiwa anakaa na kaka yake wa baba mmoja mama mmoja aitwae Alfi Mohammed Bin Almasi

Picha ya kijana aliyejifunika kashida @ kilemba ni SALUMU Mohammad enzi ya uhai wake picha ya nyeusi ni Sheikh Muhammadi Bin Abdulrahamani Alshazily babu wa marehemu nae enzi ya uhai wake picha ya mwenye joho la blue ni Sheik Nurudin Hussein Alshazily pia ni miongoni mwa mababu wa marehemu Salumu Mohammed Bin Almasi.

Unapouzungumzia uislamu wazee hawa ni miongoni mwa waliofanya kazi kuimarisha uislamu na kudumisha amani na upendo hivyo Salumu Mohammed nae alikua Imamu kwa historia ya kuzaliwa katika familia ya manguli wa Elimu ya dini ya kislamu ndani ya ukanda wa Africa Mashariki na kati huku wazee wake hawa wakiwa wamejipatia elimu ya dini kutoka nchi mbali mbali huku wakitokea Kilwa Pande. 

Kwa uwezo wa Allah wameijenga Kilwa kua na uimara wa watu wenye kumjua Mungu na kuchukua kua Dini ndiyo utamaduni wao wa maisha hata mavazi yao kua ni yakidini popote wanapokuwepo na kudumisha Amani na Upendo.

Kuvaa kanzu msuli Kilwa na kutembea na Yasin au msahafu ni sawa na Mmasai kufunga rubega au kutembea na sime ingawa kunatofauti kubwa ya kumfananisha Mmasai na mtu wa Kilwa Pande vile haijawahi Kilwa kutokea aina yeyote ya machafuko kama yatokeavyo huko kwenye jamii ya wafugaji.

Tumeamua kuweka picha za masheikh wetu hawa wawili waliotangulia mbele ya haki ili kuweka kumbukumbu sawa juu ya marehemu wetu huyu Salumu Mohammed Bin Almasi kujua ni mtu alotoka katika familia gani na kuonyesha kazi za kidini zilizofanywa na walimu wake hawa ndani na nje ya nchi hii bila kuhitirafiana na serikali au taasisi nyingine binafsi na za kidini.

Katika historia ya nchi hii watu wa Twarikat Shazily hawajawahi kuhitilafiana na serikali vile hufundisha watu Dini ili wajue kumuabudu Muumba wao.

Marehemu Salimu Mohammed Bin Almasi alishika dini na kushiriki ibada kama ilivyokua inafanywa kabla yake huku babu yake mzaa mama alofariki miaka ya 1990/91Sheikh Muhammad Bin Abdurahman Alshadhiry aliacha watoto wake na wajukuu zake WOTE kua walimu wa dini popote wanapokuwepo katika ardhi hii ya Mwenyezimungu.

Sifa ya shazily huwa anaweza kuipandisha ah'wal @ moli lakini hutokea pale tu anapokua katika dua.

Kifo cha Salimu Mohammed Bin Almasi kinaweza kuacha DOA kubwa ndani ya Shazily endapo uchunguzi hautofanyika na kupatikana majibu kwakua ni jamii iliyojijengea heshima kubwa ya uadilifu na ukalimu popote wanapokuwepo.

Njia zote za umauti hupangwa na Allah ila tukio lenye mashaka hata likileta umauti kwa mwanadamu lapaswa kubainishwa na kuondolewa shaka waziri na jeshi la polisi mutuambie kinaga ubaga ili kama tunakasoro tujirekebishe baada ya kufanya uchunguzi na si kuruhusu maiti izikwe tu na familia yake.

Narudia kidogo makala ya mchana sijawahi sikia familia ya sheikh Muhammad Bin Abdurahani ameiba hata pensel au rula darasani kama hana atakuomba umsaidie vile hana kwakua Allah amewajaalia utajiri wa imani na kusimamisha Dini ya uislamu na si fedha haya nimeyashudia tukiwa darasani na kila mwaka mwana familia yao anekuja kuanza shule kutoka familia hiyo lazima awe mwalimu wa Dini au Imamu hii Polisi pitieni kumbukumbu za familia hii katika shule walizosoma Kilwa secondary, Ndanda, Chidiya, Songea boys, Mtwara technical nk

Kubwa tunawaombea kwa Allah awaongoze KATIKA njia iliyonyooka na kuifikia pepo ya Firdausi awasamehe kwa yale yenye hitilafu ya kibinadamu.

Ndugu watanzania ifike muda tutambue Tanzania ni kubwa ina makabira mengi tamaduni nyingi hata dini pia.

Sisi watu wa Pwani ya Kilwa tumekua mfano wa kutokua na makabila huku tukitambua utaifa wetu tu na dini yetu kua hata ndiyo mila yetu na ni nguzo yetu kitaifa.

Tupeane pole wana Kilwa wote na twarikat shadhily.

Naimani kama leo masheikh wetu hawa wagekua hai ndiyo wangekua wasemaji wa hili Allah awarehemu Sheikh Nurudin Hussein Alshadhiry na Muhammad Bin Abdurahami Alshadhiry.

Pole sana Alfi Mohammed Bin Almasi najua umeumia sana kwa kuondolewa na ndugu yako ulokua unalalanae kitanda kimoja akiwa umetoka Kilwa kuja kutafuta elimu.

Allah Aqbal
Allah Aqbal
Allah Aqbal


Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD


Tazama Jinsi Rosa Ree na Emtee Walivyoshtua Watu...Huwezi Amini:

Share:
Weka Maoni yako Hapa

Total Pageviews


Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger