LOWASSA na Jeshi la Polisi Bado Ngoma Mbichi...Hili Ndilo Kosa Alilofanya....Apewa Haya Masharti

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa ameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa kwa saa nne katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi  wa Makosa ya Jinai (DCI).

Lowassa ameondoka makao makuu ya polisi saa 8.15 na kuelekea nyumbani kwake.

Akizungumza baada ya mahojiano hayo, Mwanasheria wa Chadema, Peter Kibatala amesema Lowassa amejidhamini mwenyewe na ametakiwa kuripoti tena Alhamisi saa 6.00 mchana.

Kibatala amesema Lowassa amehojiwa kwa kosa la uchochezi na ameandika maelezo ya onyo juu ya kauli aliyoitoa wakati wa futari iliyoandaliwa na mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.

"Mzee amehojiwa kwa kile wanachokiita kauli ya uchochezi aliyoitoa Juni 23, mwaka huu  wakati wa futari iliyoandaliwa na Waitara. Baada ya kuhojiwa ameandika Maelezo ya Onyo na atatakiwa kuripoti tena Alhamisi, Juni 29," amesema.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad