Breaking News: Tundu Lissu Akamatwa Uwanja wa Ndege wa Dar

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Moja ya Habari zilizotufikia kutoka Dar es Salaam ni kuhusu Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika ‘TLS’ ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria wa CHADEMA, Tundu Lissu kukamatwa na Polisi akiwa Airport Dar es Salaam akielekea Kigali, Rwanda  kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kinachoanza kesho.

Kamanda wa polisi viwanja vya ndege, Martn Ortieno amesema kwamba ni kweli wamemkamata Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa Chadema na kwamba amepelekwa makao makuu ya Polisi.

Hata hivyo, kamanda huyo hakutaja sababu za kukamatwa kwa mwanasheria huyo.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema,  John Mrema amesema kwamba mwanasheria huyo amekamatwa  jioni hii.

Mrema amesema Lissu amekamatwa na watu waliojitambulisha kwamba ni maofisa wa polisi kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu Si laisi wa chama..!! Huyu akiwalaisi Mtowe atakua nani au mnaanzisha mtafaruku katika CDM
    Huyu ni Kisu wa Singida na Yule wa Hai. sema iko njia ya shoti kati kupitia kwa mtoro na Farukwa.

    ReplyDelete

Top Post Ad