• Hot Topic

  17 Jul 2017

  Huwezi Amini..Haki za Binadamu Wadai Taifa liko Katika Kipindi Kigumu


  Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) umesema Taifa linapitia kipindi kigumu cha kuminywa kwa haki za binadamu.


  Akizungumza leo Jumapili, Julai 16, Mratibu  wa Kitaifa wa mtandao huo, Onesmo Olengurumwa amesema tangu kuanza kwa mwaka huu kuna matukio makubwa 20 ambayo yanaminya haki za binadamu.


  Amesema wakuu wa mikoa na wilaya wanakamata watu na kuwaweka mahabusu bila ya makosa.


  Olengurumwa amesema hivi sasa mtu akitoa maoni anakamatwa na kufunguliwa mashtaka kitendo ambacho ni uonevu.


  Amesema kufanya mikutano ambayo ni haki ya kisiasa inakatazwa bila ya kutolewa sababu za msingi.


  Mratibu huyo amesema mtandao unaangalia namna ya kuchukua hatua za kisheria kuhusu uvunjaji wa haki za binadamu unaofanywa na Serikali.


     

  No comments:

  Post a Comment


  Mapenzi

  Hot Gossip

  Siasa