17 Jul 2017

KIMENUKA....Aliyetobolewa Macho na Scorpion Aanza Kugawana Mali na Mkewe

WAKATI lile sakata Linalomuhusu kijana Said Mrisho aliyetobolewa macho na mtu aitwaye, Salum Njwete ‘Scorpion’ kumtelekeza mkewe, Stara Sudi ‘Mama D’ na watoto wanne, likiwa bado bichi, jipya jingine limeibuka ambapo wawili hao wameanza kugawana mali.

Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Maji-Chumvi, Tabata-Kimanga jijini Dar, zikiwa zimekatika siku chache tangu Stara apangishiwe nyumba na Said kisha jamaa huyo kwenda kuishi na mwanamke mwingine mwenye asili ya Kiarabu.
Akizungumza na Wikienda, Stara alisema kuwa amefi kia uamuzi huo wa kuchukua kilicho chake baada ya kutelekezwa kwenye nyumba hiyo.

“Amenitelekeza, nitakaa vipi hapa… nimeamua kuchukua vitu na kupeleka nyumbani kwetu. Nimekaa hapa kwa siku nne tu, nimekuja kuchukua malipo yangu ya miezi mitatu.

Ujue mwanzoni tulikubaliana na Said na akamuomba mwenye nyumba kuwa atakuwa akilipia kodi miezi mitatu-mitatu, lakini mama yangu akakataa, akasema muongo huyo, atakukimbia na kwamba kwa nini kwangu alipie miezi mitatu na kule (kwa mke mwingine) alipie miezi tisa? Said akadhani nitajua amesafi ri ili awe anakuja kwa siri kuchukua vitu kidogokidogo,” alisema Stara.

Kwa upande wake, Said alisema kuwa, alikubaliana na hatua aliyoichukua Stara ya kuchukua vitu vyote ikiwemo friji, makochi na vingine vingi, jambo lililofanywa mbele ya mashahidi akiwemo mwenye nyumba.“Nilikuwa ninatoa pesa vizuri, ilifi ka kipindi nikamwambia akatafute nyumba ya laki moja, akaenda kutafuta ya shilingi laki moja na nusu, nikalipia kwani niliomba kulipia miezi mitatumitatu.

Nashangaa kuambiwa kuwa nimetelekeza familia, hivyo ni visingizio ambavyo mwenzangu amewahi kwenda kwenye media na kuongea bila kusikiliza upande wangu,” alisema Said na kuongeza:

“Nilipigiwa simu na mwenye nyumba kuwa amepaki kila kitu kwenye gari, anahama na ameshapeleka barua Ustawi wa Jamii (Ilala) kuwa ninahitajika siku ya Jumatatu (leo) na kwamba kiasi cha kodi kilichokuwa kimelipwa (laki nne na nusu) arudishiwe kwani ndiyo kwanza amekaa miezi minne.Nilifi ka na kufanya makabidhiano mbele ya mwenye nyumba.”

STORI: MWANDISHI WETU | IJUMAA WIKIENDA| DAR

Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment


Popular Posts

Matangazo

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger