KIMENUKA...Mbunge Saed Kubenea Aitwa Polisi.......

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge wa jimbo Ubungo,(CHADEMA) Saed Kubenea ameitwa polisi na kutakiwa kuripoti leo tarehe 20/7/ 2017 kutoa maelezo kituo cha polisi kufuatia malalamiko aliyotoa Profesa Lipumba Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.

Mbunge wa Ubungo Mh Saed Kubenea wiki iliyopita alifanya mkutano na vyombo vya habari kama Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa CUF iliyochini ya uongozi wa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif na kutangaza oparesheni ya kumuondoa Profesa Lipumba katika ofisi za chama cha CUF Buguruni.
Baada ya Kubenea kutangaza oparesheni hiyo siku mbili mbele aliibuka Profesa Lipumba na kwenda kituo cha polisi kutoa malalamiko juu ya kile alichokisikia kutoka kwa kiongozi huyo na oparesheni hiyo aliyotangaza.

"Ni kweli Kubenea ameitwa na kuitwa kwake kumekuja baada ya wiki iliyopita kufanya mkutano na waandishi wa habari kama Makamu Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani akiwa pamoja na viongozi wa CUF inayoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, Julius Mtatiro na Katibu Mkuu Maalim Seif na kutangaza operesheni inayoitwa 'Operesheni Ondoa Msaliti Buguruni (OMB). Operesheni hiyo itaendeshwa kwa ushirikiano wa vyama vinavyounda UKAWA" ilisema taarifa ya CHADEMA 
Profesa Lipumba na baadhi ya viongozi wa CUF wapo katika mgogoro kutokana na kiongozi huyo kipindi cha uchaguzi mwaka 2015 kuandika barua ya kujiuzulu nafasi yake kama Mwenyekiti wa CUF taifa na kubaki mwanachama wa kawaida, lakini baada ya uchaguzi kupita kiongozi huyo akataka kubatilisha maamuzi yake ya kujiuzulu jambo ambalo viongozi wa CUF na baadhi ya wanachama wamekuwa wakilipinga na kukataa, japo  Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi yeye bado anamtambua Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF taifa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad