11 Jul 2017

Kunani East Africa Radio...Watangazi Wazuri na Ma DJ Kuondoka......

Kwa muda mrefu nimekuwa nikifuatilia Eat Africa radio na Tv, wamekuwa ni walimu kwa watangazaji wanaotoka pale yaani watangazaji wanatoka wamekwiva ki maadili hadi utendaji.

Lakini ni kama swali najiuliza ni nini kunachowakimbiza hawa watu, ni Mshahara(maslahi), kujuana, unyanyasaji kazini au ni nini ambacho wanakikimbia na wanako kwenda wanakuwa dhahabu.

Orodha ni ndefu ya walioondoka tangu enzi za Bush baby, Steve ka fire, wale naweza sema labda waliona warudi nchini kwao wakaanze maisha ya huko. Hapa kati kati walioondoka ni wengi:
Dj AD aka Mafuvu baby, Anna Peter, Allan Lucky, Michael Lukindo, Sebastian Mwaikambo, Bahati Abdul, hivi karibuni wamepata pigo na si pigo dogo hasa kwa vijana waliowatengeneza kisha wakanyakuliwa ikiwa ni Kenedy the remedy, Dj sinyorita na Mammy Babby mara upepo haujatulia Dj ambae alionekana kuziba pengo la Mafuvu nae kaenda E-fm.

Tar 8 kwenye tamasha la Komaa concert jijini Mwanza alionekana Jukwaani akisimamia shoo kwa wasanii walio alikwa hakuwa mwingine ni Dj Ommy Crazy, ambae kwa muda amekuwa hasikiki redioni (Ea radio) na alikuwa akifanya yake nilihisi jambo ila nikasema acha muda uongee.

My take Ea radio kwa sasa mna Frida au Queen fifi na King smash ni kama hadhina mliobaki nayo ni watu ambao huchoki kuwasikiliza jaribuni kuwalinda kimaslahi na vinginevo waibebe redio, radio inakosa mvuto msipo kuwa makini hao hawana muda mrefu watawapokonya.

Program meneja wa Ea radio naamini atapita hapa
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger