14 Jul 2017

Mapumziko ya Rais Magufuli Chato ni Fundisho

Kwa Mara kadhaa,watanzania tumeshuhudia Mh.RAIS wetu kipenzi cha watanzania akitumia Muda wake mwingi,Nguvu zake na Akili zake zote kuwatumikia watanzania usiku na Mchana.Ameonesha Uzalendo kwa watanzania na Taifa kwa ujumla.

Mh.Rais yupo nyumbani kwake Chato kwa mapumziko mafupi baada ya Ziara na kazi kubwa ya kujenga Taifa.Mapumziko ya Mh.Rais yanatufundisha nini?,Ingalikuwa ni Rais asiye mzalendo wa kweli,Mapumziko haya angeweza kuyafanya nchi za ng'ambo,Marekani,Dubai,Uingereza na Mataifa mengine makibwa yenye Nguvu ya Kiuchumi.

Mh.Rais,kwa kuthamini,Kujali na kutetea maslahi mapana ya kodi za Watanzania,Mh.Rais Yupo Chato kijijini kwake,Amekomaa na Tanzania yake.Najua Jamaa zetu wanatamani sana Mh.Rais asafiri nje ya nchi hata kwa siku moja tu.Lakini Mjomba ni Boda tu Boda.(Home movement).Serikali ya JPM INA sikio la usikivu sana,Kwanini imesikia ?

Vyama vya siasa vilijipatia umaarufu sana kumseama sana Mh.Kikwete na viongozi waliopita kuwa safari zao za nje ya nchi ni Matumizi mabaya ya kodi za watanzania,Chai Ikulu ni Matumizi mabaya ya kodi za watanzania,Semina na walsha ni Matumizi mabaya ya kodi za watanzania,Posho za vikao ni Matumizi mabaya ya kodi za watanzania nk,nk.

JPM,kwa hekima ,unyenyekevu na kwa Sauti ya upole akasema "NIMESIKIA KILIO CHENU" sasa everything STOP.Hakuna safari Nje ya nchi,hakuna posho,hakuna chai ya Ghalama nk,Wakaanza ooooh,Ooooh mbona Rais hasafiri nje jamani!!!!! Oooooh mbona posho hazitoki jamani!!!!!!!,Ooooh Safari za nje wabunge vipi jamani!!!!!!! nk,nk.

"Nimesikia kilio chenu,Sasa ni kila MTU awajibike sawa sawa na Maombi yake" Huyu ndiye Rais anayeendelea kugonga vichwa vya HABARI Duniani nzima kwa utendaji wake,kwa misimamo yake,kwa uzalendo wake,na kwa Uadilifu wake wa hali ya Juu.Lazima tuige mfano wa Kiongozi wetu Mkuu.

Tuendelee kumuombea matashi mema MH.Rais na serikali yake,Tuendelee kuwaombea Viongozi wetu wa chama cha mapinduzi ,Lakini tuendelee kuwaombea pia wale wa upande wa Pili ili waendelee kubatizwa kwa moto.Watanyooka tu.

Mungu Ibariki Tanzania

Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Share:
Weka Maoni yako Hapa

2 comments:

  1. Hana Makuuu Huyu, kwanza yeye anashughulika na kazi yake, wala hajishughulishi na mambo makuu, kuiba, kulibia au kuwaibia wananchi wake walio wengi masikini wa kutupwa, hana tamaa na mambo mengi ya ulimwengu huu

    ReplyDelete
  2. Basi hivi kwa akili za mtu mweusi. Anamuona kama Mjinga. Mwenzake. Wapo hapo wanaowaza ningeupata mimi hiwo Uraisi ndio muda w matanuzi na kujilimbikizia. kwa ufupi wa akili za mtu mweusi. Hasa bara hili letu la Africa. linaloambiwa watu wake wana akili kiduchu.IQ Interigent Qurty ndogo mmmmh. Ukingalia bara lote mmmmmh lakini kweli lisemwalo lipo. Manake bara kama bara lenyewe. limesheheni utajiri. Lakini wakazi wa bara lenyewe ni hoi masikini wa kutupwa asilimia kubwa. Yote hii ni kutokana na viongozi wenye akili kiduchi. IQ. intergenty Qurty ni ndogo

    ReplyDelete

Total Pageviews


Popular Posts

Matangazo

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger