RAIS wa TFF Jamal Malinzi na Wenzake Baada ya Kufikishwa Mahakamani leo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Leo July 17, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeombwa kuahirisha kesi ya utakatishaji fedha inayowakabili Rais wa TFF, Jamal Malinzi na wenzake kutokana na upelelezi kutokamilika.

Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU, Leonard Swai ameomba Mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa kutokana na upelelezi kutokamilika ambapo Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi July 31, 2017.

Rais wa TFF Jamal Malinzi, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa Shirikisho hilo, Nsiande Mwanga walifikishwa Mahakamani leo wakikabiliwa na mashitaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha Dola za Marekani, 375,418.

Aidha, Jamal Malinzi na wenzake, wamepata Mawakili wapya watatu kwa ajili ya kuwawakilisha katika kesi hiyo ambao walitambulishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Mawakili hao ni Richard Rweyongeza, Nehemia Nkoko na Abraham Senguji ambao wanakuja siku chache baada ya aliyekuwa Wakili Jerome Msemwa kujitoa kwenye kesi hiyo kwa alichodai kutopata maelekezo yoyote kutoka kwa wateja wake.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad