Aunty Ezekiel: Wema Ameleta Tumaini Jipya Najivunia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Aunty Ezekiel: Wema Ameleta Tumaini Jipya Najivunia
Msanii wa filamu bongo Aunty Ezekiel, amejivunia kitendo cha msanii mwenzake ambaye pia ni rafiki yake mkubwa Wema Sepetu, kuzindua filamu ya Heaven Sent kwa aina ya kipekee, na kusema huenda likawa tumaini jipya kwa bongo movie.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa filamu hiyo uliofanyika katika ukumbi wa sinema jijini Dar es salaam, Aunty Ezekiel amesema anaamini Wema amekuja kubadilisha tasnia ya filamu na kuwatoa shimoni wasanii hao, ambao walikuwa wanaanza kupotea kwa kukaa kimya kwa muda mrefu bila kazi mpya sokoni.
"Nimekuja kumuunga mkono Wema Sepetu ambaye amekuja na filamu mpya, naamini amekuja kuibadilisha tasnia ya filamu, labda amekuja kututoa tulipo shimoni na kutuleta juu", alisema Aunty Ezekiel.

Aunty Ezekiel aliendelea kwa kusema ...."kwa njia moja au nyingine imeleta 'bongo movie' mpya, kwa muda mrefu hakujawahi kutokea kitu kama hiki, unapoingia tu hapa unaona kabisa tasnia ya filamu inaenda kubadilika, kwa hiyo ni kitu ambacho kinanipa faraja kama msanii", aliseme muigizaji huyo.
Siku ya Jumamosi tar 26 Agosti 2017, Wema Sepetu amezindua filamu yake ya 'Heaven Sent' ambayo ilihudhuriwa na watu maarufu mbalimbli, wakiwemo waigizaji wa filamu za bongo na wa muziki pia.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad