google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Chakula Cha Kuzuia Kuzeeka Haraka...... | UDAKU SPECIAL

Chakula Cha Kuzuia Kuzeeka Haraka......

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Maisha ya sasa hivi yamegubikwa na matumizi ya vipodozi vya kuzuia uzee hadi kufikia kiwango cha kuonekana kama ni chakula kuliko vitu vya urembo. Vipodozi hivyo huja kama creams, visafisha ngozi au serums. Lakini ieleweke kuwa kutumia vipodozi vya kuondoa uzee juu ya ngozi hakuwezi kuwa mbadala wa chakula ambacho kinaboresha mwonekano na kutunza ngozi yako kuanzia ndani. Chakula cha kuzuia kuzeeka haraka ndiyo kitu muhimu katika kuufanya mwili wako usizeeke haraka na katika kuulinda mwili wako kutokana na mionzi ya UV (ultra violet) ambayo ndio chanzo kikuu cha mistari na mikunyanzi juu ya ngozi yako. Ungana nami leo kuona ni chakula gani kinasaidia kutunza mwonekano wako wa ujana.  Lakini kwanza tuvichambue vitu muhimu katika  chakula vyenye uwezo wa kulinda mwili wako usizeeke haraka.

 Vitu Muhimu Katika Chakula Vya Kuzuia Kuzeeka Haraka

 Katika mada yetu ya Ondoa Uzee tuliona kwamba mahitaji ya mwili hubadilika kadri umri unavyosonga mbele na kwamba ili kudumisha muonekano wa ujana kwa mwili wako unahitaji kuupa mwili wako mahitaji yake yaliyobadilika. Tuliona kwamba kuzuia kuzeeka haraka unahitaji chakula chenye calcium ya kutosha kuipa mifupa yako nguvu na kupata chakula chenye collagen kwa wingi ili kuifanya ngozi yako isiwe na mikunyanzi (wrinkles).

Katika miaka ya 1950 mwanasayansi Denham Harman aligundua kuwepo uhusiano mkubwa kati ya mwili kuzeeka na uwepo wa “free radicals” katika mwili wa mtu. Free radicals ni kemikali ambazo hutengenezwa na mwili katika ufanyaji wake kazi wa kawaida. Mwili una uwezo wa kudhibiti madhara yanayotokana na uwepo wa free radicals kwa kiasi fulani, lakini idadi ikizidi mwili huzidiwa na madhara mengi hutokea, yakiwepo kuzeeka kwa mwili na magonjwa mengi kama kansa, magonjwa ya moyo, arthritis, atherosclerosis, Alzheimer’s, ugonjwa wa Parkinson’s na kisukari.

Free radicals katika mwili huweza kuongezeka kwa kutumia vitu kutoka nje ya mwili. Sumu kutoka nje zinazozalisha free radicals katika mwili ni pamoja na hewa chafu hasa inayotoka kwenye viwanda, moshi wa sigara, maji na chakula chenye dawa za kuulia wadudu na utumiaji wa pombe kwa kiwango cha kuzidi kiwango.

Kiwango kidogo cha free radicals kinachozalishwa na mwili wenyewe kinaweza kikadhibitiwa vizuri na kemikali nyingine zinazoitwa antioxidants ambazo nazo pia huzalishwa na mwili. Free radicals za ziada zinazozalishwa na vitu kutoka nje ya mwili zisipodhibitiwa kikamilifu husababisha madhara mengi pamoja na magonjwa yaliyotajwa hapo juu.

Hivyo basi tunahitaji kupata chakula chenye antioxidants kwa wingi ili kuisaidia miili yetu kupambana na free radicals hizi za ziada. Kuna aina nyingi za antioxidants zilikwemo vitamini C, vitamini E, Flavonoids na Polyphenols kwa kutaja tu bila kuingia kwa undani zaidi.

Baada ya maelezo haya kidogo ya utangulizi, nafikiri sasa ni wakati mwafaka wa kupitia chakula ambacho kikitumiwa kitakupa vitu tulivyovitaja hapo juu na kuufanya mwili wako kuwa na mwonekano wa ujana daima.

 Chakula Chenye Vitamini C 

 Utafiti uliofanywa kwenye kikundi cha wanawake wenye umri wa miaka zaidi ya 40 ulionyesha kwamba wanawake wanaotumia chakula chenye vitamini C zaidi walikuwa na mikunyanzi (wrinkles) kidogo zaidi na ngozi zao hazikuwa kavu ukilinganisha na wale ambao walitumia vitamini hiyo kidogo. Hii ni kwa sababu vitamini C ni antioxidant yenye nguvu inayozuia uharibifu wa seli na DNA za seli hivyo kulinda uzalishaji wa collagen ambayo ndiyo nguzo muhimu ya kulinda ngozi yako.

 Unashauriwa basi upate angalau mg 75 za vitamini hii kwa siku. Kwa mfano unaweza kupata chungwa moja wakati wa kifungua kinywa na piliplili tano za njano ndani ya saladi kwenye mlo wako wa mchana. Chakula chenye vitamini C kwa wingi ni broccoli, strawberries, pilipili nyekundu, nyanya, tikitimaji, pomegranate n.k.

 Chakula Chenye Protini

 Tafiti zilionyesha kuwa wanawake waliotumia proteni zaidi walikuwa na wrinkles chache zaidi kwenye ngozi zao kuliko wale ambao walitumia proteni kidogo, hii kwa sababu proteni hutoa viungo muhimu katika ujenzi wa collagen.

Ili upate proteni unashauriwa kula nyama ya kuku isiyo na ngozi, sehemu nyeupe ya mayai na samaki. Unapochagua kula nyama ya ng’ombe au nguruwe, pendelea kutumia ile isiyo na mafuta sana. Matumizi ya soya yameonyesha kusaidia kuondoa ile mistari myembamba kweye macho.

 Samaki Wenye Mafuta

Samaki wa baharini wenye mafuta wamebainika kuwa na kiwango kikubwa cha “omega-3 fatty acids”, kitu ambacho husaidia kuilinda ngozi yako kutokana na mionzi mibaya ya jua ambayo hudhoofisha collagen.


Nafaka Nzima

 Utumiaji wa nafaka nzima badala ya wali mweupe, mikate inayotokana na ngano nyeupe na nafaka nyingine zilizokobolewa una faida nyingi. Moja ni kuzuia mwongezeko wa insulin katika mwili ambayo ina madhara ya kuharibu ngozi. Pia nafaka nzima ni chanzo cha madini ya selenium ambayo husaidia kuikinga ngozi yako kutokana na mionzi ya jua (UV rays).


Unashauriwa kutumia brown rice, shayiri na ngano nzima ili uweze kupata madini haya yatakayokusaidia kulinda ngozi yako.


Green Tea

Green tea ni kinywaji chenye antioxidants nyingi. Unywaji wa vikombe viwili au vitatu kwa siku wa chai hii utaifanya ngozi yako kuwa nyororo. Chai hii pia huzuia mikunyanzi isitokee kwenye ngozi yako.

Hatuwezi kuorodhesha chakula chote ambacho kinafaa katika kuzuia kuzeeka haraka katika ukurasa mmoja, hivyo makala yetu inatoa mwongozo tu wa namna ambavyo unaweza kupanga mlo wako. Usisite kutoa maoni yako kuhusu mada hii, tutafurahi mno kusikia kutoka kwako msomaji.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad