Hii Hapa Taarifa Iliyotolewa Kuhusu Kuonekana kwa Fuvu la Kichwa Katika Uwanja wa Taifa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hii HapaTaarifa Iliyotolewa Kuhusu Kuonekana kwa Fuvu la Kichwa Katika Uwanja wa Taifa
Baada ya taarifa kusambaa katika mitandao ya kijamii na picha zikisambaa kutoka uwanja wa Taifa kwa madai kuwa, kipindi hiki ukarabati wa uwanja huo sehemu ya pitch imeonekana fuvu la kichwa cha mtu, taarifa ambazo zimesambaa sana katika mitandao ya kijamii.

Mkurugenzi msaidizi wa idara ya michezo Alex Nkenyenge ili atoe taarifa kamili kuhusiana na tetesi zilizokuwa zinasambaa ni kweli ni fuvu?

“Kwanza hiyo ni taarifa ya uongo na hakuna fuvu isipokuwa ni madude ambayo yamepatikana kwenye mchanga baada ya kuwa tumefukua sehemu ya uwanja, kwa hiyo hakuna kitu kinachoitwa fuvu la mtu wala nini ni madude tu yaani mamimea yale yaliyooza basi yanafanana kama magimbi ambapo ndani lilikuwa limeshaliwa”

“Sasa kwa sababu mtu analiona kwa mbali anasema fuvu sasa sijui fuvu litakujaje hapa, kwanza kilichotokea hilo dude limekuja na mchanga wala halikuwa ndani ya uwanja, yaani kwenye mchanga uliyoletwa ambao tulikuwa tunajaza kwenye pitch baada ya kuwa tumeondoa lea ya juu”

“Kwa hiyo hakuna kitu kama hicho bahati mbaya kwa watanzania wanapenda kuzungumza vitu vibaya kuliko vizuri, maana mtu haulizi wala kushangaa ile inayosafisha uwanja, sasa kama ni fuvu unataka kusema uwanja wa Taifa kulikuwa na makaburi?”



-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad