google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Mwamuzi Mechi ya Watani wa Jadi Simba na Yanga Huyu Hapa | UDAKU SPECIAL

Mwamuzi Mechi ya Watani wa Jadi Simba na Yanga Huyu Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwamuzi Mechi ya Watani wa Jadi Simba na Yanga Huyu Hapa
Mwamuzi bora wa msimu uliopita, Elly Sassi mwenye umri wa miaka 28 ndiye atakayechezesha mechi ya watani Yanga na Simba.

Simba na Yanga zinakutana Jumatano ijayo katika mechi ya Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wa kuashiria kufunguliwa kwa pazia la ligi kuu Tanzania bara msimu wa mwaka 2017/18 utakaoanza rasmi Agasti 26.
Sassi ambaye ndiye mwamuzi bora Ligi Kuu msimu ulioisha 2016/2017.

Mwamuzi huyu kijana, amekuwa akitabiriwa kufika mbali kutokana na ubora wa kazi yake huku pia akitajwa kuwa ni mmoja wa waamuzi wenye misimamo ya kufuata sheria na kanuni za mchezo wa soka na si mtu wa kuteteleka katika maamuzi yake jambo ambalo linamfanya kumudu michezo mingi mikubwa ya ndani na nje ya nchi.

Tayari kuelekea mchezo huo mgumu mno kwa pande zote mbili yaani Simba na Yanga vilabu hivyo vyote vimekimbia jiji na kwenda kujifisha kisiwani Zanzibar, Wakati Simba wakiwa kisiwani Unguja wenzao Yanga wao wako Kisiwa cha Pemba.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad