OKWI: Nimejipanga Kuifanyia Makubwa Timu Yangu Msimu Huu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

OKWI: Nimejipanga Kuifanyia Makubwa Timu Yangu Msimu Huu
BAADA ya kufunga mabao manne kwenye mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu, mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi raia wa Uganda amefunguka kuwa huo ni mwanzo kwani amejipanga kuifanyia makubwa timu hiyo kwenye kila mchezo wake.

Okwi ambaye kwa sasa yupo kwao Uganda akiwa na timu ya taifa, The Cranes, aliifungia mabao manne Simba kwenye ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa kwanza wa ligi uliopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Okwi ambaye ameyaelekeza mabao hayo kwa mkewe, amesema kuwa ataendelea kutupia mabao kadiri atakavyoweza ili kukifanya kikosi hicho kutimiza malengo yake waliyojiwekea kwa msimu huu ya kuhakikisha wanachukua vikombe watakavyoshiriki.

“Nashukuru nimeanza vizuri ndani ya kikosi changu kwa kufunga mabao haya manne, lakini kwangu mimi bado nina jukumu zito la kuhakikisha nafunga kila niwezavyo ili kuisaidia timu kufanya vizuri.
“Yaani hapa ni mwanzo tu, mashabiki wasubiri kuona nikitupia mabao mengi zaidi na zaidi kwenye kila mchezo ambao nitashuka dimbani, nafanya hivyo ili kuleta furaha kwa mashabiki wetu kwa kuwapa makombe,” alisema Okwi.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad