Kosa Kubwa Alilofanya Diamond Platnumz Jana

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Pole sana mdogo wangu Diamond Platinum. Binafsi ni mfuatiliaji wa muziki wako na hua nadiriki hata kununua nyimbo zako katika web yako.Mimi ni shabiki pia wa Swahiba wako Ally Kiba lakini lazima nikiri kwamba umemzidi mbali sana sio meendeleo tu hata plans zako hawezi kufika hata asimame juu ya kiti itachujua miaka kukufikia ulipo.

Tuachane na hayo ndugu twende kwenye point.Kati ya siku ambazo umeonyesha udhaifu mkubwa ni jana...Hukutakiwa kabisa kwenda kwenye media kukiri kwamba umezaa na yule binti(mubeto-sijui kma nimepatia spelling)

Ulitakiwa kukomaa mpaka dakika ya mwisho kwamba hujazaa nae, hii ingekusaidia kutunza heshima yako pamoja na kuimarisha ndoa yako.Wanawake wanaamini sana maneno kutoka kwa mwanaume.Zarinah asingeweza kukwambia kapime DNA hata kama mtoto angetoka copy right na wewe.Mwanamke ni mwepesi sana kusamehe kuliko mwanaume.

Kama ni kweli ulishamwambia Zari kuhusu mtoto wa nje basi hukua na haja ya kwenda kuatangaza aisee.Ona sasa kila mtu hata watoto wadogo wamejua kwamba ulimsaliti mkeo(japo not official) lakini navojua huu mwaka wa nne kama sio wa tatu uko na huyo mama(zarinah).Wanawake wanataka heshima, wanataka kuthaminiwa.Ikiwa umeweza kwenda na yule mdada chumbani unapolala na yule mama hataweza tena kukuamini.Umemvua nguo kabisa aisee.Hana hamu tena ya kuja Tz, yale mapicha picha airport sidhani kama atapiga tena.

Zile show off zenu nadhani hazitakuwepo tena.Naanza kuona mwisho wa uchumba wenu.

Sasa yule mama atakugeuza anavotaka.Tegemea kulia sana katika swala la mapenzi.

Mdogo wangu bado kidogo ufikishe miaka 30.Karibu sana katika umri huu kijana.Sisi wengine tuna uzoefu sana katika haya mambo.Hata tukutwe live tunakana kwamba sio kweli na tunasamehewa.

Sina hakika kama ushauri wa wewe kwenda kwemye media uliutoa kwa Babu tale ama fella.

Maana naamini wao ni wajuzi zaidi wa haya mambo na hivo wasingekushauri kwenda kutangaza kama vile unaomba msamaha watanzania.

Sisi tunaweza kukusamehe lakini yule mama hawezi kabisa.Atakutesa sana mi nakushuri bora uachane nae kabisa aise.Tegemea kuona mapicha ya uchi na clips za mitombo akiwa na majamaa halafu uchune tu maana tayar ushamchafua kwa hiyo atalipiza.

Kumbuka hana cha kupoteza hata akiachana na wewe.Yeye sio hao wanaotaka elfu 70 kwa siku yeye anapesa yake.

Ulitakiwa kuomba ushauri kwa wakubwa na wazoefu wa mambo kabla hujaenda kukiri mbele ya watanzania mil 24 wapiga kura wenye akili timamu na above 18 waliokua leo hii wanakuangalia unapuyanga.
Tegemea heshima yako kushuka sana mwaka huu.

Mubeto hana tofauti na akina Giggy na amber lulu sijui, ambao ni kama day-waka.Kwamba apate deal ndio aingize mkwanja au afanya vibiashara vidogo vya mission town apate mshiko.

Sasa hivi atakufanya wewe kitega uchumi.Nimesikia umesema anataka mil 5 kila mwezi(What)?.kwa maana nyingine ni kwamba kale ka faidi kote kwenye biashara zako za nguo atakua anachukua mubeto.

Hili ni kosa kubwa sana na pengine siku hii hutaisahu.Hakukua na haja yoyote ya wewe kutangaza ingebaki kama tetesi tu.

Hata kama alivujisha picha, you could tell zarinah kwamba , she was ma chick by then kwisha!.Kwani wanagapi wana zalishwa na kuachwa wanakua ma single mother?.

Kama mtoto si unao wawili?.Ulishindwa nn kumhudumia kimya kimya.Alichotaka yule mubeto ni kujulikana kwamba kazaa na wewe lakini pia alipata sapoti kubwa kutoka kwa ma x wako, huu mchezo uliujua lakini umeingia king.Wao daima hawafurahi kabisa wewe kua na yule mama maana ni kama vile umewadharau baada ya kuwamega na kuwaacha.So lengonlao uharibikiwe na ndo wanafanikiwa hivo.

Kulikua na maandalizi ya kufungua kesi kwamba umemkana mtoto lakini pia ungeweza kumhudumia mtoto but sio kwa mil 5 kwa mwezi!

Unaenda kufilisika bro niamini.Najua utasema kwamba oohh unapiga hela ndefu lakini siongelei hela naongelea saikolojia yako kwa sasa itakunyima raha miaka na miaka na hii itakutafuna niamini.

Na kama ikitokea yule bibi akaghairi ushirikiano na wewe please usije kufanya kosa kumrudia yeyote kati ya wale ulioisha wapitia.Hawatakua na jipya zaidi ya kukufilisi, ni bora umfuate yule wa big brother kama ni kweli ulimpiga pia. Aisee ila na wewe hatari.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mwandishi huna jipya yule c mkewe zari ni hawara wake na hakuna ndoa baina ya mktristo na muislamu bora kama anataka kuowa atafute muislamu mwezaka Allah ( s.w) atamuliza ujana wake katumia vipi ktk maisha ya dunia

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hujui maana ya ndoa na hawara pia hata tfaut hujui ktk misingi ya kisheria. Zari ni mke wake na hakuna maelezo tfaut na huo ukwel. Sasa km zari ni hawara na huyo mobeto ni nani. ACHA KUITA WAKE ZA WATU MAHAWARA KWA KICNGIZIO CHA DINI. AU na ww una stress za kike km hao Wanaomtukan zari tena bila sababu.

      Delete
    2. Hata wewe hujui maana ya neno ndoa, sasa nasema tena kwa herufi kubwa na wewe ukisoma soma kwa sauti "WOTE ZARI NA MOBETO NI HAWARA ZAKE" Usipingane na ukweli... Ndoa ni maneno mawili kwa mafunzo ya dini yetu "Mtu anapoambiwa nime kuozesha naye kisha kujibu NIMEMUOA" Kama hilo halija fanyika basi ni wazinifu tu hata wewe kama hujaoa kupitia mafunzo ya dini yako BASI JUA UNAZINI TU...

      Delete
  2. ONCE MWANAUME ANAPOWAGONGANISHA WANAWAKE UWE TIYARI KUDONDOKA KIMAISHA HATA KAMA NI KIMAENDELEO, MIMI SIO SHABIKI WAKO DIAMOND ILA JARIBU KUWAKWEPA HAWA WANAWAKE.UMKAA NA ZARI UKAENDELEA SANA NA HATA KUWA VIWANGO VINGINE, USIDHANI KILA MWANAMKE ANA NYOTA YAKO WENGINE WATAKUJA NA NYOTA ZA PUNDA RESULT TO KUJUTA NA KUPOROMOKA. KUMBUKA ULIKOTOKA NA HAPO ULIPO. EPUKA WANAWAKE KAMA UNAVYOEPUKA UKIMWI. MI NI MWANAMKE ILA SIKUSHAURI KIENDEKEZA WANAWAKE WATAKUHARBIA MAISHA, UTAISHI KIJINGA.KILA MKONO WA MWANAMKE UNA BARAKA ZAKE . UTACHEKA LEO NA MABUSU JUU KESHO ATAKUKIMBIA HATA BUSU HATOLIKUMBUKA. ATAENDA KWA WENYE HELA.

    ReplyDelete
  3. Ni kweli dimond ulikosea pale ulipoenda kwenye media kuweka mambo yako ya ndani hadharani. sikatai haya makosa ya kuwa na mtoto nje yapo, hata kama umekubali mtoto ni wako haya mambo yanafanywa kimya kimya sio lazima upige tarumbeta hasa ukizingatia wewe ni kioo cha jamii. sio ukiwa star basi kila jambo lako unaliweka hadharani. mambo mengine hayapaswi kuwekwa hadharani hasa kwa jamii yetu ya kiafrika. jifunze nini cha kuongea hadharani na kipi hakifai kuwekwa hadharani. kaa chini na wahenga watakufunda ipasavyo.

    ReplyDelete
  4. KAMA NI KUTOKEA ISHATOKEA NA MUNGU AMESHAMSAMEHE DIOMOND KWA KUSEMA UKWELI NYIE MNAOTAKA AFICHE HIYO NI DHAMBI,MI NAMSHAURI TU KWANZA DINI YAKE INARUHUSU KUWA NA WAKE MPAKA WANNE YEYE KAMA ANAWAPENDA WOTE AAMUE TU KUFUNGA NAO NDOA NA INAWEZEKANA KWANZA KWA MTAZAMO WANGU TU D ANAONYESHA KABISA ANAMPENDA HAMISA NA WALA SIO KWAMBA NI KUZAA TU SO MAAMUZI NI YAKE.

    ReplyDelete
  5. Diamond hajakosea kitu. Kafanya uzinzi kapata mtoto na mtoto ni damu yake. Sasa afiche nini mtoto wa Hamisa na kwa nini aweke wazi watoto alozaa na Zari? Hamisa na Zari wote ni wanawake ambao wametumiwa kimapenzi na Diamond kwani hakuna hata mmoja ambaye ni mke haki kwa Diaomnd. Kama kuficha angekuwa anajidanganya tu nafsi yake kwani sio yeye na Hamisa peke yao ndio waliokuwa wanajua, mama Diamond na dada yake Diamond walikuwa wanajua, of course na upande wa akina Hamisa utakuwa unajua sasa hapo kipi kinafichwa!!! Ni bora kuweka wazi yeye mwenyewe kuliko kupitia third part. Maoni ya wengine yanaonyesha kuwa Zari kama ndie mwanamke sahihi kwa Diamond na wengine siwo. Muonyeni huyo Diamond aache tabia ya UZINZI na sio kusema kuwa kakosea kuweka upumbavu wake bayana

    ReplyDelete
  6. cha ajabu nini mbn munatu shangaza kwani ni wa kwanza daimond kuzaa nje hakuanza yeye na wala hato kuwa wa mwisho au huyo zari povu likutokee ninj umeje sahau daimind alikuwa na wema ukumnyakua wewe sasa kelele za nini

    ReplyDelete
  7. Diamond hakufanya makosa; yeye anawajua wanawake wote wawili, na inawezekana kabisa hana mapenzi ya dhati kwa Zari bali kwa show off, na sasa ameona basi. Hii siyo mimba yake ya kwanza kwa Hamisa, nyingine ilitoka mwaka jana, ndipo akaweka tena hii, kwa hiyo siyo bahati mbaya. Kabla ya kukutana na Zari, Diamond alikuwa akiandaa ndoa yake na msichana ambaye hakuwa maarufu wakati huo, na Zari alimvaa Diamond akiwa desparate sana kufanikisha pati yake ya white party, ndipo akatumia alicho nacho kumvuta Diamond na baada ya pati akawa ana mimba! je mipango ya harusi ya Diamond iliishia hapo? hatujui. Mwaka jana ilikuwa waachane baada ya safari yao ya Ulaya, lakini Zari akatangaza kuwa ana mimba nyingine. Naona tusimkose Diamond wakati hatujui nyuma ya pazia; inawezekana sasa amefikia kikomo upande ule anataka kuelekea upande mwingine.

    ReplyDelete
  8. Suala halikuwa kwamba Diamond alitakiwa kuficha bali kosa lake lilikuwa ni kutumia media kutangaza/kukiri kuwa mtoto ni wake! Mimi si shabiki wa Diamond ila nampenda kwa sababu moja jamaa anajua kutafuta/mjasiriamali amepata mafanikio makubwa katika maisha yake akiwa katika umri mdogo tafsiri yake ni kuwa anasafari ndefu mbele yake, nimesikia hata miaka 30 hajafikisha, Kwa watu waliosoma Historia watajua kuwa Empire rise and Fall, Diamond is like ana EMPIRE na sasa hii Empire ipo katika kilele chake sasa tukitumia historia maanguko hayako mbali, na kama wanazuoni wa mashariki walivyosema "Everytime History repeats itself the price goes up" simuombei mabaya huyu bwana mdogo, ila kuna mambo anatakiwa ajifunze kama vile dunia inavyokwenda "DOMINO EFFECT" One wrong move and everything falls apart. Leo watu wanakupenda na kukujadili siku ukianguka yatakuwa ya MR. NICE utasahaulika wataangalia nani anasumbua kwa wakati huo. Don't prove to people they are right prove to them they are wrong. All the best with your next wrong move!

    ReplyDelete
  9. Usimdharalishe mke wako. Kufunga ndoa au siyo. Nanyi wanawake wengine mnaojipeleka. Ujue. Hupo bora kuliko mwanamke wa ndani wa huyu bwana. Kama Diamond hajui namna ya kumheshimu mama mtoto wake sababu ya utajiri, umaarufu au jingine. Ujue mtu wa namna hii hatakosa kushuka. Zari kafanya mengi sana kwa Diamond. Where ever you see successful man there is a very strong successful and inteligent woman behind him. Kama hajui angoje. Muombe radhi Zai kwa heshima zote, na ujue kufunga zip yako.Ingekuwa mwanamke wangekuita malaya. Unamwitaje mwanaume ambaye hajui kuifunga suruali yaka wakati wote yupo uch?

    ReplyDelete

Top Post Ad