Msigwa: Chama cha Mapinduzi Kimechoka Polisi Acheni Kukisaidia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msigwa: Chama cha Mapinduzi Kimechoka Polisi Acheni Kukisaidia
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kulitaka jeshi la polisi nchini kutokisaidia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema wamuache yeye na CHADEMA wapambane kukiondoa chama hicho madarakani kwani kimeshachoka

Msigwa amesema kitendo cha polisi juzi kumkamata wakati akiwa kwenye majukumu yake ya kibunge kimemuudhi sana na kusema ni jukumu la Mbunge yoyote yule kuelimisha jamii, kuwapa habari wananchi pamoja na kuikosoa serikali.
"Mimi nilikuwa sifanyi uchochezi kazi ya Mbunge kuelimisha, kuhabarisha, kuikosoa, kuisimamia serikali na kuchochea maendeleo katika jimbo kwa hiyo kama Mbunge ninayo haki ya kuzungumzia Demokrasia na haki ya kuzungumzia mambo ya utawala bora, nina haki ya kuzungumzia haki za binadamu , kitendo cha polisi kunikamata juzi kimeniudhi sana hao polisi waniache mimi na chama changu tupambane na CCM, wasiisadie CCM kwani saizi imechoka ipo dhohofu yaani ipo taabani wanajaribu kuitetea CCM, wajitokeze CCM wenyewe wajibu hoja" alisema Msigwa
Msigwa aliendelea kusema kuwa yeye ni Mbunge ana haki ya kuikosoa serikali iliyopo madarakani hata kuichonganisha na wananchi ili wasiichangue tena mwaka 2020 anadai huo ndiyo wajibu wake kisiasa na ndiyo maana anakuwa mpinzani.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mfyuuuuuuuu.....nani atakujibu....??? Ukibishana na mwendawazimu na wewe pia watadhani ni mwendawazimu...nyinyi semeni, tukaneni mchana usiku mtalala, hata hao polisi kuwakamata hao wendawazimu ni kuwanenepesha mibichwa yao tu, hebu waacheni, wapotezeeni muone kama hawatachoka kuchonga.....msonyooooooooooooo

    ReplyDelete
    Replies
    1. msonyoooooooooooooooo mwingine mfyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu wakalale hawajielewiiiiiiii imebaki mipayukajiiiiiii tena mfyuuuuuuuuuuuuu

      Delete
  2. Kabisa...mnawapotezea Tu.
    Ila wakigeuza Mara ikawa ya kichochezi. Pale haraka...una react

    ReplyDelete
  3. ni vizuri mkajipanga, kusema CCM imechoka wakati madiwani wenu wanhamia huko siyo sahihi, jipange

    ReplyDelete

Top Post Ad