Ukomo wa Umri wa Rais Pasua Kichwa Uganda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ukomo wa Umri wa Rais Pasua Kichwa Uganda
Kikundi cha wafuasi kindakindaki wa chama tawala cha NRM wakiwemo baadhi ya wenyeviti wa majimbo wameelezea pendekezo la kufuta Ibara ya 102 (b) ya Katiba ili kuondoa ukomo wa umri wa rais ni jaribio la kupindua sheria mama.

Wafuasi hao wanasema wazo la kuondoa ukomo wa umri wa mgombea urais linachochewa na uroho

Katika taarifa yao iliyosomwa jana na Dennis Sekabira, ambaye ni mwenyekiti wa Jimbo la Nakaseke Kusini, kikundi hicho kiliwaambia waandishi wa habari kwamba wanapinga msimamo wa wabunge wa chama hicho kwa sababu mradi wao huo hauna maslahi kwa amani ya nchi.

“Huu ni mwelekeo hatari na unahatarisha amani tuliyoifaidi nchini,” alisema Sekabira ambaye ameeleza kwamba kikundi hicho kina wajumbe 121 wa Halmashauri Kuu ya Taifa, chombo cha pili kwa ukubwa katika uongozi wa chama.

Mwenyekiti huyo alisema wajumbe hao hawaungi mkono juhudi za kuzuia maoni ya wengi dhidi ya kusudio la kuondoa ibara hiyo na kwamba inahitajika amani wakati wa kukabidhi madaraka.

“Tumeamua tusiinyime haki nchi yetu nafasi pekee ya kubadilisha mamlaka kwa amani,” alisema. “Badala ya kuhutubia suala la ukomo wa umri, wabunge wa NRM wanapaswa kujikita katika utekelezaji wa Ilani ya chama.”

Mwaka 2015 Waganda walibadili katiba kuondoa ukomo wa mihula kumwezesha Rais Yoweri Museveni kugombea muhula wa tatu na kuendelea na sasa ukiondolewa ukomo wa umri wa miaka 75, rais huyo mwenye umri wa miaka 73 sasa atakuwa huru kugombea tena mwaka 2021 akiwa na umri wa miaka 77.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ukimuangalia kwa macho tu unajua fika kuwa jamaa ana roho mbaya na roho za watu wasio na makosa/hatia yeyote ulizozitoa uhai ipo siku utalipa hapa hapa duniani angalia dictator mwenzako Iddi Amin mwisho wake ulivyokuwa zamu yako na wewe itafika tu "YOU CAN RUN BUT YOU CAN'T HIDE YOURSELF"

    ReplyDelete

Top Post Ad