Baba Diamond: Nitakufa na Mobetto na Migogo Yao Hayawezi Kunifanya Nimchukie

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baba Diamond: Nitakufa na Mobetto na Migogo Yao Hayawezi Kunifanya Nimchukie
BAADA ya hivi karibuni mwanamitindo Hamisa Mobeto kumpeleka mahakamani msanii wa Bongo Fleva kwa madai ya malezi ya mtoto aliyezaa naye, baba wa msanii huyo, Abdul Juma ameibuka na kusema hata iweje, yeye atakufa na mkwewe huyo kwani hayo mengine ni ya kwao, hayamhusu.
Akipiga stori na Risasi Jumamosi, mzee Abdul alisema anachojua yeye, Hamisa ni mkwe wake aliyempa heshima na kumtambua kama baba mkwe wake hivyo hata mwaliko aliompa wa kwenda kwenye sherehe ya mwanaye huyo aliyepewa jina lake la Abdul atakwenda kama kawaida kama atakuwepo, hajali kama wamepelekana mahakamani wala nini.

“Hayo mambo ya migogoro yao hayanihusu kwa kweli na hayawezi kunifanya nikamchukia Hamisa kwa kuwa ni ya kwao, nikiwepo Dar lazima niende kwenye sherehe ya mjukuu wangu Abdul wala sijali chochote,” alisema mzee Abdul.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Big up mzee Abdul kwa kweli umenifurahisha

    ReplyDelete

Top Post Ad