Godbless Lema Adai Gari lake Limechomolewa nati 13 na Watu Wasiojulikana

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Gari la Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema  limechomoka matairi leo Jumatatu baada kudaiwa kuwa limefunguliwa nati 13 kati ya 20 na watu wasiojulikana.

Lema amesema walikuwa wamepanga na Mbunge wa Arumeru Mashariki(Chadema), Joshua Nassari kuondoka na gari hilo jana usiku kuelekea Dar es Salaam kuwasilisha ushahidi wa tuhuma za rushwa za madiwani waliohama Chadema.

Hata hivyo amesema majira ya mchana alipokuwa na gari alihisi mlio kwenye tairi ndipo alikwenda kuliegesha hoteli ya Equator.

Amesema kutokana na kulitilia shaka gari aliomba lifti kwenye gari la Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli, Isack Joseph kwenda naye Dar es Salaam.

"Asubuhi leo (Jumatatu) nikamtuma dereva wangu akachukue gari Equator hoteli alipeleke gereji na baada ya kutoka mita chache tairi zilichomoka," amesema.

Amesema tayari amemuagiza dereva kwenda kutoa taarifa polisi lakini ameiomba kampuni ya  ulinzi ya inteligence inayolinda nyumba yake kufanya uchunguzi kubaini watu walioingia ndani na kufungua nati.

"Pia nimeomba wataalam kupitia kamera za nyumbani kwangu kuona kilichotokea kwani kuna uwezekano wa watu kuingia ndani kufanya uhalifu huo.”

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad