Mdee Mdee Noma Amjibu IGP Sirro Sakata la Sheik Ponda na Polisi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge wa Kawe kupitia CHADEMA, Halima James Mdee, amejibu kauli ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Nyakoro Sirro ya kutojadili suala la Tundu Lissu, na kusema hawatoacha kufanya hivyo.

Kwenye ukurasa wake wa twitter Halima Mdee ameandika ujumbe akisema kwamba hakuna sheria inayokataza mtu kujadili jambo fulani, na IGP hana mamlaka ya kukataza hilo.

“Hakuna popote katika sheria za nchi IGP ana mamlaka ya kunyamazisha watu wasijadili jambo, tutaendelea kujadili ya Lissu mpaka haki itendeke”, ameandika Halima Mdee.
Pia Halima Mdee ameendelea kwa kuandika kuhusu kukamatwa Sheikh Ponda, akisema ni mipango ya kuwafunga mdomo watu watakaojadili suala hilo.

“Najaribu kutafakari alichokisema Ponda na kwa namna gani kinaashiria uchochezi, sikioni! ni namna ya kutisha na kufunga midomo watu”, ameandika Halima Mdee.

Hivi karibuni IGP Sirro aliwataka wanasiasa kuacha kufanya mijadala ya kumjadili Tundu Lissu, na waliache jeshi la polisi lifanye kazi zake bila kuingiliwa na jana Jeshi la polisi lilitoa agizo kwa Shekh Ponda kufika kituo cha polisi kutokana na kauli alizozitoa juu ya sakata la Tundu Lissu.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. na kweli kwa nini wanakataza watu kuongea au kujajadili shekh Ponda hajaongea kitu kibaya wala hajaongea maneno ya uchochezi kabisa jamani mbn tanzania imekuwa hivo inatisha watu wana ogopa hata kuweka uwekezaji baadae tena tusikie nyumba za fulani zimetaifishwa tunaogopa hebu bunge likae lijadili lifafanue maneno ya uchochezi ni yapi? this is very scary

    ReplyDelete

Top Post Ad