Mrisho Gambo: Sina Tatizo na Lema ila Inabidi Asome Alama za Nyakati

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mrisho Gambo amefunguka na kusema Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema anapaswa kutambua kuwa yeye kama Mkuu wa mkoa anajishughulisha na matatizo ya watu hivyo kama hatabadili aina ya siasa azifanyazo  basi anapoteza muda wake kwa miaka mitano yote.

Gambo amesema kuwa yeye hana tatizo lolote na Mbunge huyo wa Arusha mjini na kudai kwamba anapaswa kutambua na kubadili aina ya siasa anazofanya kwa kuwa yeye amelenga kutatua matatizo na changamoto za watu wa Arusha Mjini.

"Msuguano na Mbunge haupo lakini anatakiwa tu asome alama za nyakati kwamba Mkuu wa Mkoa wa sasa amedhamiria kuhangaika na shida za watu kama hatalitambua hilo atapoteza muda wake kwa miaka yake yote mitano" alisema Mrisho Gambo.

Aidha Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa yeye kama kiongozi kijana anahitaji zaidi kukosolewa kuliko kusifiwa ili aweze kujirekebisha sehemu ambayo ana mapungufu ili aweze kuwa kiongozi madhubuti na mahiri zaidi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad