Nape Apigilia Msumari Kauli ya Msekwa 'Hichi Ndicho Chama cha Julius Nikijuacho'

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nape Apigilia Msumari Kauli ya Msekwa 'Hichi Ndicho Chama cha Julius Nikijuacho'
Mbunge wa jimbo la Mtama, Mh Nape Nnauye amepigilia msumari kauli iliyotolewa na Spika wa zamani wa Bunge , Pius Msekwa kuhusu miaka ya uongozi na kusema misimamo hiyo ndiyo misimamo ya Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwalimu Julius Nyerere.

Nape Nnauye ameweka video ya Pius Msekwa akielezea juu ya ukomo wa kiongozi madarakani na kusema chama hicho kilishafikiria miaka ya nyuma kuongeza miaka kutoka 10 na kuendelea lakini waliona miaka kumi inatosha kwa mtu kuongoza na kusisitiza ikiwa miaka 15 ikatokea mkapata kiongozi mbaya miaka hiyo itakuwa ni mingi sana.
"Miaka 15 mkipata kiongozi mbaya ni mingi sana, nashauri ibaki miaka 10 kama kiongozi ni mbaya angalau tumvumilie kwa miaka 10 tu halafu basi ndivyo hoja ya miaka 10 ilivyopita si kama hiyo mingine hatukufikiri ilifikiriwa ndiyo maana naposikia kuna Mbunge mmoja anataka kupendekeza twende kwenye miaka saba kwa vipindi viwili ninataka kumjulisha kwamba hili si wazo jipya tulishafikiri na lilikataliwa kwa hiyo mimi na imani CCM itaendelea kulikataa hilo, tutabaki kwenye miaka mitano tu mara mbili basi" alisisitiza Msekwa
Kufuatia kauli hiyo ndipo Nape Nnauye alipigiria msumari na kusema hicho ndicho Chama Cha Mapinduzi (CCM) cha Mwalimu Julius Nyerere anachokijua yeye, siku za karibuni Mbunge wa Chemba (CCM), Juma Nkamia alidai anataka kupeleka hoja bungeni kuongeza muda wa utawala hadi miaka 7 badala ya miaka mitano ya sasa.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na sisi pia ndio Chama tunachokijua 5 inatosha .

    ReplyDelete
  2. Lakini hayo ni mawazo yake J. Nkamia, anao uhuru wa kutoa mawazo yake kama wengine, mnaona kama kioja, kwani vepe?? hahahah! au ni sababu ya JPM ndio mapovu yanawatoka, hata hivyo JPM mwenyewe alishasema uraisi ni mzigo, jinsi TZ ilivyo-oza, anajuta kugombea, tena aliweke wazi kabisa hana mpango wa kuongeza muda, sasa nini tena,,,,,,,,KWA KIPINDI HICHO KIFUPI, MTANYOOKA TU! tehe tehe tehe

    ReplyDelete
  3. na bado WATANYOOKA SANA povu povu "hata hivyo JPM mwenyewe alishasema uraisi ni mzigo, jinsi TZ ilivyo-oza, anajuta kugombea, tena aliweke wazi kabisa hana mpango wa kuongeza muda, sasa nini tena???,,,KWA KIPINDI HICHO KIFUPI, MTANYOOKA TU! haa haa haa haa haa haa haa..MAGU OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE...

    ReplyDelete

Top Post Ad