Nassari: Maisha Yangu Yapo Hatarini..Aliowaanika Mchana Kweupe Wanamtafuta

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki (CHADEMA) Joshua Nassari amefunguka na kusema maisha yake yapo hatarini na kudai kuwa watu ambao amewaanika kwenye sakata la ununuzi wa madiwani wanamtafuta.

Nassari amesema hayo ikiwa imepita siku moja toka alipokwenda kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kupeleka ushahidi wake juu ya madiwani wa CHADEMA waliohama chama kwa kuhongwa rushwa na wateule wa Rais John Pombe Magufuli.

"Maisha yangu yapo kwenye bonde la uvuli wa mauti, Maisha yangu yapo hatarini kwani Watesi wetu wananitafuta" aliandika Nassari kupitia ukurasa wake wa facebook

Mbali na hilo wachangiaji mbalimbali kwenye ukurasa wa Mbunge huyo walimtaka azidi kumuomba Mungu huku wakimshauri kuongeza ulinzi zaidi katika maisha yake ya kila siku kutokana na jambo ambalo ameliibua na kumtaka aendelee kupambana, baadhi ya wachangiaji wengine wamedai kuwa anachofanya ni njia ya kujitafutia umaarufu kisiasa.

Juzi  Mbunge Joshua Nassari, Godbless Lema pamoja na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa walikwenda kwenye Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kupeleka ushahidi wao juu ya sakata la kununuliwa kwa madiwani wa CHADEMA na kuhongwa fedha na ahadi mbalimbali kutoka kwa wateule wa Rais mkoani Arusha.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivi hii ni kweli ama kiki?? Inawezekaje Muheshimiwa Diwani 'ajisalimishe' CCM sababu ya shilingi millioni 2!! Mbona kama haingii akilini......vipi na yule Diwani wa Iringa, alihongwa na nani?? Hebu tuwache movie iendelee.......

    ReplyDelete

Top Post Ad