Prof. Kitila: Wizara yangu itamsaidia Rais Magufuli kupata kura nyingi bila kampeni katika uchaguzi wa 2020

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo ameahidi kuwa wizara yake itakuwa mfano bora wa kumsaidia Rais John Magufuli ili apate kura za kutosha bila kufanya kampeni mwaka 2020.

Profesa Mkumbo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wawakilishi wa viongozi wa mamlaka 19 za maji kuhusu mipango mbalimbali ya kuboresha sekta ya maji nchini.

Amesema ahadi yake haitakwenda bure kwani mwaka 2020 Rais Magufuli ataanzia Dar es Salaam hadi Kigoma akipunga mkono tu bila kusema neno lakini kura zitakuwa za kishindo.

Katibu huyo amesema Wizara ya Maji ndiyo kila kitu kwani inawagusa wananchi wa hali ya chini na juu na ndiyo maana kuna ulazima wa kuwa na usimamizi wa kutosha.

Kutokana na hilo Profesa Kitila amekemea tabia ya vyama vya wafanyakazi kutengeneza majungu ya wivu na kugeuza mamlaka za maji kuwa vichaka vya majungu na umbea ambapo matokeo yake ni kuumiza na kuwabambikizia tuhuma viongozi wakiwemo wakurugenzi wa mamlaka hizo.

Amewataka wafanyakazi kupigania haki zao huku wakitimiza wajibu wao kwani bila wao kufanya kazi kwa tija hawawezi kuwa na haki ya kudai maslahi bora.

Katibu wa kikao hicho Robert Chilewa amesema mamlaka hizo zimekuwa na changamoto kubwa kutokana madeni yanayofikia Sh 15 bilioni kutoka taasisi na mashirika ya umma.

Amesema mamlaka zimeanza kuyumba kwa utendaji kazi kutokana na kuondolewa kwa watumishi wasiofikia elimu ya kidato cha nne ambao walikuwa nguzo imara huku Wilaya ya Wanging'ombe anakotoka Waziri wa Maji ikiwa na watumishi asilimia 72 wote wa darasa la saba na akamwomba Profesa Kitila awasaidie watumishi hao warudishwe kazini.

CHANZO: Mwananchi
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe ni kiongozi wa serikali. Ulikuwa upinzani kupigania haki, uhuru, uwazi. nawashangaa viongozi kama nyinyi. Sijui unaelimu gani ya juu. Lakii acha elimu. Unaingilia mambo ya siasa kama aliyekuchagua na ni upotoshaji mkuu kitaifa kwa Watanzania wote hasa wasio na elimu na wasiojua kutofautisha serikali na sisa za vyama. Hapa inaonekama mojakwa moja unalipa . Unamlipa Raisi kwa kukuteua na kumpigia debe moja kwa moja. Na huu ni upotofu kwa umma, na inakuwa kama ni rushwa pia. Inasikitisha sana huku kuyumba kwa viongozi wanateuliwa na kutokujua na kuheshimu mipaka kikazi. Si ni utovu wa adabu tu, inaonyesha nchi kutokupevuka kielimu. Elimu duni kwa viongozi wetu wengi ndio chimbuko la matatizo mengi nchini. Sasa kama walioelimika wanafanya hili je asiye na elimu na ni wengi sana itakuwaje? utakuta hawa ndio wakwamishaji wa maendeleo kwa kutokuwa na uwezo wa kufikiri na uhuru wa kujichagulia. Inabidi Watanzania wote tupigwe msasa kisiasa, na kiuzalendo ili tujue tupo huru kujialia, kujichagulia na kusema unalolifikiri na kuliamini bila woga.
    Bado njia ndefu. Ni miaka 15 Taifa limejipotezea haya. Viongozi wetu chini ya chama Tawala waliachiwa huru sana kujitafutia maslahi binafsi na ndugu zao kupitia vyeo vyao na ukaribu wa kisiasa kupitia Maraisi na mawaziri. Sasa Tuna mtu anajitahidi, lakini hata hivyo hawezi kulitatua hilo bila kukaa sawa na kuwasikiliza hasa wapinzani ambao kwa miaka yote hii kazi zao ilikuwa ni kuleta taharuki ya kukionyesha chama Tawala kilivyokwenda nje ya maadili kulitokomeza Taifa. Ndo maana wanaitwa Wapinzani na wanaonekana ni maadui pale wanapoyaibua Mfisadi, wadanganyifu, wapokeaji na watoa rushwa. Wanaonekana eti hawaungi mkono harakati za raisi. Wanaziunga sana bali kwa vile wako mitaani na kuyaona yale wau toka chama tawala hawaendani na na yale yasemwayo na ndgugu magufuli wanawekwa ndani na kushambuliwa kila siku.Sasa tuuone usikivu wa raisi baada ya mambo mengi kuletwa hadharani, tuone ataamua vipi kwa kuliepusha Taifa hili lisiangamie zaidi ya hapa.
    MUNGU IBARIKI TANZANIA. MUNGU AMPE VIPAJI ndugu Pombe ili aweze kushukiwa na hekima ya hali ya pekee kuonyeshwa hili kama kweli nia yake ni kutumbua bila kunjali mtu yeyote, cheo, kabila au nini. Najua anayasoma haya. Hizi sifa toka UN, haziisaidii Nchi hii. Wanakupuliza maji uweze kuwapa zaidi utajiri wa nchi hii. Nchi hii itajengwa na Wazalendo Watanzania. Si Wachina, Si Wamarekani, si Waingereza, na si Wafaransa. Jiulize, kwa nini wanakusifia sana.Wanataka nini kwako.Hawawezi kuijenga Tanzania na kuacha kwao. Bali Watahakikisha Wataitumia Tanzania, na Watanzania kwa maslahi yao binafsi na kuondoka nayo.
    Lini Waafrika tutajitawala , kujichagulia, na kuchagua nini kinamanufaa kwetu na si wanavyotuletea maombi ya uwekezaji kama wanavyofanya. Tanzania haiwahitaji Wachina kutuamulia tujenge Dubai kule wanakojenga sehemu ya bandari. Kama mnafikiri ile ni sehemu kuu za kuingiza na kutoroshea viyu, na kuchezea kamali. Huwapi wageni sehemu ya bandari kwa mambo haya. Ungewapa Dodoma si Kule. Wachina wezi wakuu. Mtakuja juta karibuni tuu. Ni kati ya miradi itabidi ipitiwe na kueguliwa haraka sana. Natoa Tahadhari kubwa kwa serikali ya Magufuli. Katika kuchimba watahamisha utajiri wa hali ya juu msioufahamu bure tu. Tafadhali liangalieni hili kwa mapana sana. Mbagala si kwa kuuzwa.

    ReplyDelete

Top Post Ad