Rais Magufuli Awapa Onyo Wakuu wa Mikoa, Makatibu 'Sitaki Nisikie Mtu Anasema Yeye Mgeni'

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais Magufuli Awapa Onyo Wakuu wa Mikoa, Makatibu 'Sitaki Nisikie Mtu Anasema Yeye Mgeni'
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amewaapisha Makatibu Wakuu na Wakuu wa Mikoa ambao amewateua hapo jana.

Sherehe hiyo ambayo imehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kitaifa akiwemo Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu, Jaji Mkuu  Ibrahim Hamis Juma , Spika wa Bunge Job Ndugai na wengineo, imefanyika katika ukumbi wa Ikulu jiini Dar es salaam.
Baada ya kuwaapisha viongozi hao Rais Magufuli amewataka kwenda kufanya kazi kwa bidii na weledi, huku akitoa onyo kali.
"Nyinyi ni wawakilishi wa Watanzania, mkawe watumishi wao, mkawe sauti yao, mkamtangulize Mungu, wakuu wa mikoa mkaangalie kuna vitu gani ambavyo mnaweza kufanya katika kubadilisha uchumi wa eneo lake, wote mlioteuliwa sitaki nisikie mtu anasema yeye mgeni, tunataka maeneo yenu muyajue. Najua mkitoka hapa wengine mtakwenda kusherehekea wengine mtakwenda kupewa pole, mkafanye kazi", amesema Rais Magufuli.
Sambamba na hilo Rais Magufuli amemuhamisha Mkuu wa mkoa mpya wa Dodoma Bi. Christine Mndeme na kumpeleka mkoani Ruvuma, na yule ambaye alikuwa mkoani Ruvuma kutakiwa kwenda kuripoti mkoani Dodoma mara moja.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad