Wabunge Kupewa Donge Nono la Fedha Ili Kutoa Ushauri Ukomo wa Umri wa Urais

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wabunge Kupewa Donge Nono la Fedha Ili Kutoa Ushauri Ukomo wa Umri wa Urais
Kila mbunge anatarajiwa kupewa kiasi fulani cha fedha zitakazomsaidia kupata ushauri kwa wapigakura jimboni kwake kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria wa 2017 unaolenga kuondoa ukomo wa umri kwa wagombea urais.

Baada ya muswada huo kusomwa kwa mara ya kwanza na Raphael Magyezi, mbunge wa Igara Magharibi kutoka chama tawala cha NRM, kisha kupelekwa katika Kamati ya Kudumu ya Sheria na Huduma za Bunge, Jumanne Spika Rebecca Kadaga aliwataka wabunge kwenda kushauriana na wapigakura wao.

Baada ya uamuzi huo wa Spika, mnadhimu mkuu bungeni Ruth Nankabirwa amesema Tume ya Bunge inafikiria kutenga bajeti maalumu kwa ajili ya kuwarahisishia wabunge.

“Tume ya Bunge inajiandaa kutengeneza bajeti kwa sababu ni Bunge ambalo litaturahisishia sisi sote …Tutaelezwa ni kiasi gani na namna gani kila mbunge atapata na kwenda kushauriana kwa sababu tunahitaji usafiri,” Nankabirwa ameviambia vyombo vya habari.

Nankabirwa hakuweka wazi undani wa bajeti hiyo akisema tu kwamba Tume ya Bunge ndiyo itapanga na kubainisha kiasi kinachohitajika. Lakini mbunge wa Kakumiro kutoka NRM, Robinah Nabbanja ambaye ni mjumbe wa Tume ya Bunge alisema mgawo huo utakuwa kwa wabunge wote bila kujali vyama vyao.

“Tutakutana haraka na kukubaliana. Sitaweza kukutajia kiwango kwa sasa kwa sababu bado hatujakubaliana. Huwezi kuwatuma wabunge (kupata ushauri) bila kuwawezesha kiasi,” amesema Nabbanja.

Kuhusu suala la wapi fedha hizo zitatoka hasa ikizingatiwa hazijatengwa katika bajeti ya sasa, Nabbanja amesema watapunguza kutoka kasma ya safari za nje.

“Jambo lolote linapokuwa la dharura, kwa kawaida huwa tunagusa fedha za usafiri wan je, tunaweza kuhamisha vifungu ndani ya bajeti,” amesema.

Mnadhimu wa kambi ya upinzani Ibrahim Ssemujju amepuuza uwezeshaji huo akiuelezea kuwa ni jaribio la “kusafisha rushwa kwa wabunge”.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tz baadh ya waandishi ni wacenge wa akili. Kitu chochote lazima kiwe na kichwa na kuhusu habari, kichwa cha habari ndio habari yenyewe lakini baadhi ya vichwa vya habari vya waandishi ni mavi matupu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tena ni mambumbu au mazumbu kuku, yasiyo na akili, kwanza lazima uwandike habari umeitoa wapi, na kichwa cha habari na tukio lenyewe limetokea wapi? Nadhani Tanzania tuna elimu ya chini sana na katika hii sekta, hata ukiwa mwandishi wa blogg bado uwe na mantikkk ya kueleweka Idiot

      Delete

Top Post Ad