Baada ya Takukuru Kutangaza Donge Nono Hatimaye Mhasibu Wake Ajisalimisha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baada ya Takukuru Kutangaza Donge Nono Hatimaye Mhasibu Wake Ajisalimisha
Aliyekuwa Mhasibu mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na  Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey John Gugai amejisalimisha katika taasisi hiyo.
Akizungumza na Mwananchi leo Novemba 15,  Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishna Valentino Mlowola amesema Gugai amejisalimisha na hatua za kisheria zinaendelea.
"Ni kweli amejisalimisha na yupo chini ya vyombo vya ulinzi na usalama na hatua zaidi za kisheria zitafuata" amesema Kamishna Mlowola
Mtumishi huyo anatuhumiwa kujipatia mali kinyume cha Sheria za Utumishi wa umma huku Takukuru wakidai kwamba kama atadhibitisha uhalali wa umiliki wake ataachiwa na akishindwa atachukuliwa hatua.
Gugai amejisalimisha ikiwa ni siku moja imepita tangu Takukuru ilipotangaza zawadi ya Sh 10 milioni kwa mwananchi yoyote ambaye angefanikisha kumtia nguvuni mtumishi  huyo.
Hata hivyo, Kamishna Molowa ameshindwa kufafanua kama amejisalimisha mwenyewe au kuna mtu katoa taarifa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad