Masha Aomba Kutumiwa Pale Atakapohitajika

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Masha Aomba Kutumiwa Pale Atakapohitajika
Aliyekuwa mwanachama wa CHADEMA Lawrence Masha ambaye ametangaza kukihama chama hiko hivi karibuni, ameomba kurejea CCM na kutumiwa pale atakapohitajika.

Akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri Kuu cha CCM kinachoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais Magufuli, Masha amesema yeye ni kada wa CCM kwani amezaliwa na kukulia kwenye CCM, hivyo anaomba uongozi wa CCM umkubalie aweze kurudi nyumbani na kuitumikia CCM.
"Mwaka 2015 nilifanya maamuzi ambayo sina sababu ya kueleza sana, nimezaliwa ndani ya chama hiki, nilipohama ilibidi nimfiche mzee Masha, akanipigia simu akanuliza umefanya? nikamuuliza kwani wewe chama gani? akaniambia mimi nilifukuzwa we umehama, amefurahi sana juzi nilipomwambia narejea CCM, Mheshimiwa Mwenyekiti na kamati yako, naomba mnikubali, naahidi nitakuwa mwaminifu kwa chama cha Mapinduzi na serikali yake, ukinihitaji nitumie", amesema Lawrence Masha.
Hivi karibuni Lawrence Masha alitangaza kukihama chama cha CHADEMA akisema chama hiko hakina nia madhubuti ya kushika dola kama malengo ya vyama vya upinzani vingi duniani.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad