UVCCM Wamvaa Mbowe, Wasema Rais Magufuli Hajawahi Kutamka Mahali Popote Kama Serikali ni ya Kwake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

“Rais Dk John Pombe Magufuli hajawahi kutamka mahali popote kama Serikali ni ya kwake na si ya CCM kama ilivyodaiwa na kiongozi wa upinzani Bungeni Freeman Aikael Mbowe” – Shaka

“Pamoja na Serikali kuongozwa na Rais Magufuli bado iko chini ya Chama Cha Mapinduzi na kumtaka Mbowe kuacha maneno ya upotoshaji na uchochezi wa kitoto” - Shaka

“Rais Dk Magufuli tokea alipoingia madarakani miaka miwili iliopita amekuwa akihimiza shime ya kukuza fikra mpya na kudumisha uzalendo ulioporomoka na kuzaa kundi la mafisadi, wezi wa mali za umma bila kujali itikadi za kisiasa kwasababu uzalendo hauna alama ya siasa au chama” - Shaka

“Matamshi ya Mbowe hayana msingi wala mantiki yoyote bali anaonekana kama mtu anayeweweseka usingizini baadaa ya kuona utendaji wa Serikali ya CCM kwa miaka miwili ukiendeshwa kwa uwajibikaji, ufanisi, umakini na kuweka pembeni mitazamo hafifu ya kisiasa huku ikijali zaidi nchi na utaifa” – Shaka.

"Mbowe ni mwanasiasa mnafiki na profesa wa kuzua. Amesahau alipowakusanya wananchi pale Mwembeyanga Temeke na kutaja orodha ya viongozi wa Serikali aliodai ni mafisadi likiwemo jina la Edward Lowassa aliyehamia Chadema na kuteuliwa kuwa mgombea urais " - Shaka.

“Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 /2020 ni miliki ya ya CCM na Rais Dk Magufuli hana ilani binafsi ya uchaguzi hivyo Mbowe aache kumlisha maneno Rais kwa kusaka kwake umaarufu dhaifu wa kisiasa.” - Shaka

"Mbowe aache kufuatilia mambo ya CCM kwasabahu hayatamsaidia yeye au chama chake. Hana sifa ya kuwa kiongozi mkweli mbele ya Watanzania kwa sababu ni wakala wa mafisadi na chama chake kimekuwa maficho ya viongozi wasiotamanika katika jamii " - Shaka.

“Serikali ya awamu ya tano haijawahi kukataa kupokea ushauri au maoni ndiyo maana Rais Dk Magufuli amekubali hata kupokea ilani ya uchaguzi ya ACT Wazalendo na madai ya kuteua viongozi kwa mtazamo wa udini, ukabila au ukanda huo ni upuuzi usiohitaji kusikilizwa.” - Shaka

“CCM itaendelea kuamini na kufuata itikadi ya siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kama ilivyoanishwa kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani ujamaa si utitiri wa vibanda vya nyasi na kadhia ya umasikini bali ni imani na utekelezaji.” - Shaka

“Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kwa umakini na uangalifu mpya ili kukwepa yaliotokea nyuma yasijirudie tena na kukuta faida au tija ya rasilimali za Taifa zikiwanufaisha Mabepari na Mafisadi.” - Shaka

“Ninachokiamini kwa mujibu wa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020, Serikali haijaibeza sekta binafsi, kupuuzia uwekezaji na wawekezaji au kutofungua milango ya ushirika wa maendeleo bali kinachowatatiza baadhi ya Mafisadi na Wanasiasa uchwara ni kuzibwa kwa mirija na mianya ya wizi wao.” - Shaka

"Kiongozi yeyote anayekuwa wa kwanza kuumwa au kuthubutu kuutaja udini na ukabila hadharani huyo ndiye mkabila na mdini halisi. Hatuwezi kuteua viongozi kwa kutazama idadi ya makabila, dini au ukanda kwasababu Serikali si kilenge cha mizimu na matambiko" - Shaka.

“Nasikitishwa na matamshi ya Mbowe kudai hali ya uchumi ni mbaya wakati takwimu za uchumi katika taasisi za kitaifa na kimataifa zikiutaja uchumi wa Tanzania kukua kwa kasi.” - Shaka

"Huwezi kuwahimiza waumini wa Kikristo au Waislam kufanya ibada ikiwa hakuna Misikiti au Makanisa. Tunajenga viwanda, tutazalisha ili kupata masoko ya ndani na nje kutokana na ubora wa bidhaa. Hata Wachina, Waingereza na Wamarekani hatukukubaliana kama tutanunua bidhaa zao" - Shaka.

“Rais Magufuli na Seikali inayoongozwa na CCM itaendelea na mikakati yake katika dhamira ya kujenga uchumi imara wa viwanda kuelekea uchumi wa kati, kuziba mifereji ya wizi na ufisadi bila kuyumbiswa na mayowe ya wapinzani.” – Shaka

Shaka Hamdu Shaka ni Kaimu Katibu Mkuu UVCCM ameyasema hayo alipozumgumza na waandishi wa habari ofisini kwake huko Upanga jijini Dar es Salaam kufuatia madai ya Mbowe dhidi ya Rais na utawala wake.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. EEE CCM. Kamwe hamtabadilika, hata mkiona mabadiliko ya kweli. Mtawatetea wachache badala ya Watanzania walio wengi. Nasikitika kuona kundi la watu, kumvamia kiongozi wa chama cha upinzani namna hii. Watanzania, Ebu vijana wa sasa turudi na tufikiri , nchi yetu toka tupate uhuru. Ni chama kimoja bila mabadiliko. Hata mkiwa wakali namna hii mabadiliko yanaingia polepole. Watu wanafuatilia hasa kwa ukaribu. Bila upinzani nchi hii ingeuzwa yote. Lakini, CCm haiwezi kuona makosa yao. Wengi mnataka vyeo, badala ya kuwatumikia watu. makelele bila hoja za msingi, ni makelele tu. Ni wimbo wa kila siku. Watu wanataka Katiba, Sheria moja kutumika kwa wote na si kwa wachache au kwa kichama. Mafisadi wote walioitafuna Tanzania wako CCM. Hivi hamjiulizi. mbona hamuwatumbui walioweka mikataba, Walioingiza mali nyingi bila kulipa kodi, Waliotaifisha mali za umma na kugawana kindugu, kichama mpaka mabenki. Wenye accounti nje mmelima kabisa hili. Sasa mnachokipigia kelele ni nini. Nani alitoa loliondo ya Wamasai, Nani alitoa ardhi kwa wawekezaji huko Serengeti kupitia mazingira badala ya kuwapa Wamassai walioishi huko miaka nenda rudi. Mkiwa na nia yote mabovu ni CCM mmeyafanya. Leo mnawapigia kelele Wapinzani. Mungu lete amani nchini badala ya chuki na uongo. Mungu wafungue vijana ambao wanataka kupoteza ukweli wa mambo. Kwa Watanzania wengi wazalendo mnaofuatilia siasa kwa sasa, najua wengi waoga, lakini Mungu katupa zawadi nchi tukufu na kila kitu. kilichokosekana ni Uzalendo wa kweli, demokrasia, ushujaa na upendo wa kweli kwa kila Mtanzania. Tukiwa na upendo haya yote hayangetokea. Ubinafsi ni mwingi mno.

    ReplyDelete

Top Post Ad