Miili ya Askari Waliokufa DRC Kurejeshwa Kesho na Serikali, UN

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Miili ya Askari Waliokufa DRC Kurejeshwa Kesho na Serikali, UN
Serikali inashirikiana na Umoja wa Mataifa (UN) kuhakikisha miili ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliouawa na waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) inarejeshwa nchini.

Akizungumzia na waandishi wa habari jana, mnadhimu mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali James Mwakibolwa alisema miili ya askari hao itarejeshwa nchini kati ya Jumanne na Jumatano. Mwakibolwa alisema askari hao walivamiwa kambini na waasi wa kundi cha ADF na mapigano yalidumu kwa takriban saa 13.

Alisema askari 14 wa JWTZ waliuawa, 44 walijeruhiwa na wengine wawili hawajulikani walipo.

Mwakibolwa alisema tukio hilo lililotokea Desemba 7 katika kambi ndogo iliyopo kwenye daraja la Mto Simulike lililopo Kaskazini Mashariki mwa Wilaya ya Beni, Jimbo la Kivu.

Alisema shambulio hilo ni kubwa zaidi kutokea tangu JWTZ ianze kushiriki ulinzi wa amani nchini DRC mwaka 2011.

“Taratibu za kusafirisha miili ya marehemu kuirejesha nchini inafanyika chini ya uratibu wa Serikali na Umoja wa Mataifa. JWTZ na Serikali tunaendelea kuchukua hatua stahiki kufuatilia tukio hili ikiwamo kufanya uchunguzi katika eneo husika,” alisema Mwakibolwa.

Alisema tukio hilo halitawavunja moyo JWTZ wala kutetereka kupeperusha bendera ya Tanzania ndani na nje ya nchi bali linawaongezea ari, nguvu, ushupavu na uhodari zaidi katika kutekeleza majukumu yao.

“Ni bahati mbaya mashujaa wetu wameuawa wakiwa wanatekeleza jukumu la ulinzi wa amani nchini DRC. Kwa umoja wetu Watanzania tuwaombee dua roho zao zipumzike kwa amani na majeruhi wapone haraka iwezekanavyo ili warejee kutekeleza majukumu yao,” alisema.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad