Mr Nice Amruka Young Dee " Sijawahi Kumruhusu Binadamu Yoyote Kutumia Kazi Zangu Bila Makubaliano"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mr Nice Amruka Young Dee " Sijawahi Kumruhusu Binadamu Yoyote Kutumia Kazi Zangu Bila Makubaliano"
Msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva kwenye miondoko ya TAKEU, Mr. Nice, amesema hamjui msanii Young D ambaye ametumia wimbo wake, na kwamba hakubaliani na kitendo cha yeye kutumia kazi yake.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Teolevision, Mr. Nice amesema licha ya kutoruhusu mtu yeyote kutumia kazi zake, hajapata taarifa kutoka kwa Young D wala uongozi wake, na hajawahi kumjua kwenye maisha yake.
"Sijawahi kuongea wala kuruhusu binadamu yoyote kutumia kazi yangu yoyote bila makubaliano na ridhaa yangu mwenyewe iwe ni kwa kuniheshimu ama kunidhihaki, so far simjui huyo Young D at all , ndo namsikia kwako", amesema Mr. Nice.
Kwa upande wa Young D amesema suala hilo tayari uongozi wake unalishughulikia ili kumalizana na malalamiko ya Mr. Nice, hata hivyo aliamua kufanya kama kumpa heshima kutokana na kukubali kazi zake alizokuwa akizifanya.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad