UKAWA Yafunguka Kuhusu Serikali ya Awamu ya Tano

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA umesema kuwa umejiridhisha kuwa Serikali ya awamu ya Tano sio serikali ambayo inafuata utawala bora,  kuzingatia haki za binadamu huku ikivunja katiba.

Akizungumza na  waandishi wa habari, Mwenyekiti mwenza wa Umoja huo,  Freeman Mbowe amesema vipo viashiria vingi vinavyoonesha kuwa uongozi wa awamu ya Tano hauzingatii katiba ikiwemo kuzuia mikutano ya kisiasa Pamoja na kushambulia Kwa viongozi wa vyama vya upinzani.

" Serikali inabana wazi  kuzungumzia na kuikosoa,  hata nyinyi wandishi hampo Salama, ndio maana mwenzenu azory Mpaka sasa hajapatikana na serikali haijatoa tamko lolote" amesema Mbowe.

Mbowe pia alizungumzia uchaguzi mdogo wa madiwani ambapo Kata 43 zilifanya uchaguzi huku ccm ikishinda Kata 42 na Chadema walishinda moja.

Alisema viongozi  wao wakiwemo wabunge, madiwani na wagombea wa upinzani walikua wakikamatwa na kuwekwa ndani huku wasimamizi wao wakitolewa nje ya vyumba vya Kura jambo ambalo ni kinyume na katiba ya nchini.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hula lako Bao Nbowe. Na Siasa Za Kuokota Zimesha kushinda kama yule mwenzako Jito Zubeli

    “Wapinzani siyo tu wanapotezana, bali hadi sasa wameshapotezana, tumeshawapiga 4-0 ugenini na tukirudi nyumbani nako ni 4-0, tunamaliza kazi, CCM Oyee!!” – Oyeeeeeeee... CCM MBELE!!!!
    Mbele kwa Mbele

    ReplyDelete
  2. Si kweli. Mtaona mnashinda kwa sasa. Ni wale ambao ni dhaifu, wamebanwa. wana njaa na hawana himiri na ushujaa pekee ya kusimama wima kupigania maslahi ya Taifa zima na watu wa kawaida. Mtu huwezi kuina CCM malaika baada ya kupigwa, watu kutekwa, kupoteza maisha, kukataza mikutano, kupigwa mabomu . Wengi waliodharalika ni kama wamefyata mkia.
    Kuna tofauti ya kufyata mkia na kusimama shujaa na kuwa tayari kutoa mhanga kwa manufaa ya Taifa. Kinachoniuma hasa ni kitu kimoja. Hawa watu kupurutika baada ya kumwona Lisu kukaa kitandani , kunusurika kifo, na kumbwaga. Akina Wema, Akina Kafulila, mwenyekiti wa bachva. Mungu kamnusuru Lisu, Akimrudishia nguvu za kutembea tena, sijui watamsogelea tena, watamcheka, watamkejeli sijui. Ni hawa nawaita boys, ni ishara moja watakimbia kumwacha mke wao, mtoto afe akishambuliwa na kumtelekeza. Mioyo yao inasema vingine tofauti ni vinywa vyao. Huu ndo ukweli halisi wa nchi yetu. Haina mshikamano, haina uzalendo, na bado watu hawajui uzalendo ni nini. Imani ya ndani ya mtu, hata ukimuunga raisi kwa matendo yake, lakini pia unapima utashi, hekima, ukweli, ushujaa, uwazi, na ujasiri halisi kikazi kuwaadhibu wote hasa vinara bila woga. Lakini ingawa Ndugu magufuli anajitahidi, kamwe hatashinda. Sababu, kawaachia viongozi wakuu wa ngazi za juu ambao nao wamo katika hujuma hizi wakisaidiana na hawa papasi, na watu wa kati ambao bado wapo huru, wapo CCM, wamepewa kinga, na wengine wanaogopwa. Wapo kwenye madawa, Madini, mikataba, Ardhi, wanyama kutoroshwa. Na hawa wanazuia kufubguliwa mashataka baadhi ya mawaziri, na wengine. Bado wanamiliki walivyojimilikisha. Na wanatengeneza pesa kupitia miradi, pesa waliziiba, majumba, na wengine wanaubia katika gesi, migodi, mbuga na mengi tu. Je utautokomezaje ufisadi kwa mazingira ya namna hii? Ebu tuambieni.

    ReplyDelete
  3. Mbowe ... kama unajifanya hujui au hutaki kuelewa..
    Sisi tutakuambia.
    Sakozi yako na matumizi na uzulumaji wa Posho ukishirikiana na baadhi ya waliohamia hapo ...Wana chedeme wameistukia Picha hii mbovu.
    Baafda ya kupata maasfa ktk hii sakozi...Imefika wakati ujiulize....!!! na ukae na Utafakari
    Je haya yananitokea mimi Chanzo na Sababu yake ni nini.

    Ikiwa hawa wa karibu wamenifanya kama Msaliti wa awali kwangu sito kuubeli Kambwe.
    Je mimi hatima yangu ni Nini?
    Hapo utajiuliza tena Je na Nchi/Watanzania wananielewaje mimi katika kupokea na kutumia Ruzuku nnayo pewa kama sakozi/Chame.

    Freman... Nakuomba uwe na Amani na Ujisikie Free Man. Na uanzishe biashara nyingine ambayo sis siasaa manake wewe Si mwana sasa wala umahiri wa Jambo hili zaidi ya kuleta Taharuki na Sitofamu
    Kwa nchi na wananchi ili upate kiki...Mie nakushauri mtembelee Nguza Karl Bond atakupa Michongo wa wakati wa sasa... cha kufanya.
    POLE FREMANI MBOWE . JE KWENU KUNA NGOMBE KAMA EDO
    MWENZAKO EDO , HIVI SIKU ZA USONI ATATOA UAMUZI NA KULUDI KIJIJINI AENDELEE NA UZALISHAJI.
    WEWE MWENZANGU NA MIE ... INAKUWAJE SASA....GOLESI TULIKUWA NAE NIA KAONESHA ILA ANANGOJA WAKATI MUAFAKA TU....
    SHAULI YAKO... USIJE KUSEMA HATU KUKUTAHADHARISHA. KAA CHONJO SAA MBAYA.
    SPIDI NA UTENDAJI WA HUYU GAME CHANGER MAGU HAMUIWEZI. WENZAKO WANA WEWESEKA.
    MWENYEKULA DIKLOFENAKI WENGINE PALASETAMOLI.. JE WEWE UTAKULA NINI ASPILINI???

    ReplyDelete

Top Post Ad