Ulega afanya ziara ya kushtukiza soko la Samaki Mwanza

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwanza. Naibu Waziri wa Uvuvi, Abdalla Ulega, leo Ijumaa amefanya ziara ya kushtukiza katika soko la kimataifa la samaki la Kirumba jijini Mwanza na kukamata tani 11 za samaki waliokuwa wakiandaliwa kusafirishwa nje ya nchi kinyume cha sheria.

Shehena hiyo ya samaki  ambao hawaruhusiwi kuvuliwa kisheria, wanadaiwa kuwa walitaka kusafirishwa kwenda nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) kupitia mpaka wa Rusumo mkoani Kagera.

Pamoja na kukamata samaki hao, naibu waziri huyo pia ameagiza kuondolewa mara moja kutoka sokoni hapo maofisa uvuvi kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela waliokuwa na dhamana ya kusimamia ukaguzi katika soko hilo kwa kushindwa kutimiza wajibu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huu ndio uchapa Kazi sahihi tunao utaka.
    Hii ni hatua Sahihi ya kumsaidia Raisi wetu JPM.
    asie wajibika katika Dhamana Aliopewa na kukaribisha Ubadhirifu. Asivumiliwe ni nje tu. Mpaka waru kuwa Waaminifu.
    Hapa Kazi tu......TANZANIA KWANZA...KUILETA TANZANIA YETU MPYA NI LAZIMA TUBADILIKE.

    ReplyDelete

Top Post Ad