BREAKING: Rais Magufuli aongeza baraza la mawaziri, Amteua Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Januari, 2018 amemteua Mhe. Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini.

Mhe. Doto Mashaka Biteko ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe na  alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya muda iliyochunguza madini ya Tanzanite.

Kufuatia uteuzi huu Wizara ya Madini sasa itakuwa na Waziri na Naibu Mawaziri wawili.

Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi huu kwa lengo la kuongeza nguvu kutokana na uwingi wa majukumu katika Wizara ya Madini.

Mhe. Doto Mashaka Biteko ataapishwa Jumatatu tarehe 08 Januari, 2018 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Januari, 2018
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sawa Baba JPJM.
    Umetathmini ukubwa wa Malengo na kupata Jibu.
    Unagawa majukumu in a coordinated sphere of responsibility.
    Kwa nia Na Lengo kuwa Rasilimaali ya Tanzania italindwa na Mtanzania
    kwa Ajili ya Kumnufaisha Mtanzania.

    Mungu akuweke BABA. WATAKUELEWA TU KADIRI SIKU ZINAVYOENDA.

    ReplyDelete

Top Post Ad