Hii Hapa Kauli ya Zitto Kabwe Baada Kuzuiwa Kufanya Mkutano na Polisi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hii Hapa Kauli ya Zitto Kabwe Baada Kuzuiwa Kufanya Mkutano  na Polisi
January 16, 2018 Mbunge Kigoma Mjini na Kiongozi wa chama cha ACT wazalendo Zitto Zuber Kabwe ameonesha kutokuridhishwa na uamuzi wa  jeshi la polisi mkoani Kigoma baada ya kuzuia Mkutano wa hadhara wa Mbunge huyo.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Zitto Kabwe ameandika “Jeshi la polisi limezuia Mkutano wangu wa hadhara kama Mbunge wa Kigoma Mjini kinyume na sheria ya Bunge ya mwaka 1988. Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge inayolazimisha  Mbunge kufanya mkutano kwenye jimbo lake bila vikwazo”.

“Sitaki kuwapa polisi sifa ya kupambana nasi. Tumeghairisha mkutano mpaka siku ya jumamosi, tumewaandikia barua rasmi kuwa sheria waliyoinukuu sio sheria halali na haihusiani na mikutano ya Mbunge kwenye jimbo lake. Sheria wanayopaswa kunukuu ni sheria namba 3 ya mwaka 1988 kifungu cha 4(1). “- Zitto Kabwe

 “Ofisi yangu  itamwandikia Spika wa Bunge rasmi kuhusu suala hili ili lisifanyike kwa Mbunge mwingine yeyote”. -Zitto Kabwe

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Angry Face bado yupo yupo tu. katika anga za ulingoni.
    Wenye chama wote wameshamuondoka kabaki peke yake. Anasikitisha..!!!
    Rudi kigoma kuvua Dagaa na kuimarisha Soko.

    ReplyDelete

Top Post Ad