Sumaye: Taifa Linaelekea Kubaya Viongozi Wanatakiwa Kusimamia Haki

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Sumaye: Taifa Linaelekea Kubaya Viongozi Wanatakiwa Kusimamia Haki
Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye amewataka viongozi nchini kusimamia haki kwa maelezo kuwa Taifa linakoelekea ni kubaya.

Sumaye ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani amewaomba viongozi wa dini kutokaa kimya na kuwataka kukemea maovu yanayoendelea kwani ni jukumu lao na si siasa.

Amesema hayo leo Februari 20,2018 katika Kanisa la Mtakatifu Anna, Hananasif, wakati wa misa ya  kumwombea Katibu wa Chadema, Kata ya Hananasif, Daniel John.

Akitoa salamu za Chadema, Sumaye amesema "Daniel hakufa kwa kuipigania haki, amekufa kwa kupigania haki. Baba paroko nakuhakikishia hii si siasa. Chumvi inapokosa radhi hutupwa nje."

"Haki haitendeki, maumivu yanatokea na tunanyamaza, tunapaswa kutupwa nje na kukanyangwa kanyangwa, Daniel amekuwa chumvi hivyo ametupwa nje," amesema

Akisisitiza, Sumaye amesema "Katika kupigania haki, kuna wachache watamwaga damu, Daniel ni miongoni mwao na hao  hawatarudi, hakuna historia hiyo popote damu hiyo itadai itadai."

Sumaye ameongeza "Taifa lote tukemee na wahusika wakachukua hatua zinazopaswa sina hakika kama zitachukuliwa, pale tunapozipuuza, tukaona hawachukuliwi hatua, siku damu zitakapodai hakuna wa kuizuia."

Kuhusu viongozi wa kiroho, Sumaye ameaema "Viongozi wa dini kemeeni, mnapoona kuna ubaya halafu hamsemi, hii si siasa, kemeeni ni jukumu letu sote na msipokemea taifa hili linakwenda kubaya."

Amesema Mungu ampokee huko kunakostahili na sisi turejee katika mstari na kuwa nia njema yenye amani

Sumaye amesema Chama kimesikitika sana kwa yote yaliyotokea na tangu msiba ulipotokea tumekuwa na familia na tutaendekea kuwa nao mpaka tutakapomsindikiza katika makazi yake ya milele.

Sumaye amesema Mungu anahusika na uhai wetu lakini sisi binadamu tunafanya mambo yasiyostahili.

Akitoa salamu za watu waliokuwa wakifanya kazi kwa ukaribu zaidi ni Severine Kimario amesema zilikuwa taarifa za kushtua kuhusu kifo chake lakini mwisho wa siku kazi ya Mungu haina makosa.

John aliyezaliwa Desemba 26, 1980  , altekwa, kipigwa na kuuawa na watu wasiojulikana Februari 11,2018 kisha mwili wake kutupwa fukwe za Coco.

Baada ya misa, mwili wa John unasafarishwa kwenda Mafinga mkoani Iringa kwa mazishi. John ameacha watoto wawili na mjane mmoja.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria misa hiyo ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara, Profesa Abdallah Safari, Meya wa Ubungo, Boniface Jacob, mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na mbunge wa Viti Maalum, Susan Lyimo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad