Viongozi Chadema Wawasili Kituoo Kikuu cha Polisi, Waachiwa kwa Dhamana

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Viongozi Chadema Wawasili Kituoo Kikuu cha Polisi

Viongozi watano wa Chadema kati ya saba waliokwenda Kituo Kikuu cha Polisi kuitikia wito wa kamanda  wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, wameachiwa kwa dhamana. 

Walifika kituoni hapo leo Februari 20, 2018 saa 6: 10 mchana na kuachiwa saa 7:45 mchana.

Viongozi walioitwa na Mambosasa ni mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, katibu mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji, manaibu katibu wakuu (bara), John Mnyika na Salum Mwalimu (Zanzibar).

Pia wamo, mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee; mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti, John Heche na Ester Matiko ambaye ni mweka hazina wa Bawacha.

Jana, Mambosasa aliieleza MCL Digital kuwa viongozi hao ni watuhumiwa na kama wameitwa polisi ni fadhila tu, ila kwa yaliyotokea wanapaswa kukamatwa.

Waliofika kituoni hapo ni Bulaya, Mdee, Matiko, Heche na  Mnyika

Wito wa viongozi hao polisi umekuja siku siku nne tangu kutokea kwa kifo cha Akwilina Akwiline, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Taifa cha Usfairishaji (NIT).

Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo vya mawakala wao.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad